Saturday, 6 July 2013

tata mandiba




Uwezekano wa kuishi  muda mrefu "MANDIBA"Mandela?


Afya ya Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela maarufu kama tata mandiba Mwaka 1994, Reagan aligundulika kuwa na ugonjwa wa Alzheimer uliomweka hospitalini. Alifariki baada ya miaka 10 akiwa hospitalini. imeendelea kudorora, ikiwa ni siku ya 29 sasa tangu apoteze fahamu.
Masikio na macho yote ya vyombo vya habari duniani yameelekezwa nchini Afrika ya Kusini, huku kila chombo cha habari kikiwa mstari wa mbele kuelezea mwendelezo wa hali yake.
Kila chombo katika mtazamo wake, waandishi wa habari pia wamekuwa wakielezea mitazamo yao juu ya afya ya Mandela. Wapo wanaoona kuwa mwisho wake umekaribia, pia wapo wanaoamini anaweza kuinuka siku moja na kumudu kazi zake mwenyewe.
Hata hivyo, licha ya mitazamo hiyo ukweli ni kwamba mwenye mamlaka dhidi ya kesho ni Mwenyezi Mungu pekee na ndiye anayefahamu ni lini siyo tu Mandela bali hata wewe unayesoma makala haya kuwa utaondoka katika ulimwengu huu.
Wakati kila mmoja akiwa na mawazo yake juu ya hatma ya Tata Madiba, unafahamu kuwa wako walioweza kuishi kwa muda mrefu wakiwa katika hali kama yake ?
Najua ungependa kujua kama inawezekana kuishi katika hali hiyo kwa muda mrefu.
Baadhi ya viongozi waliokuwa katika hali kama ya mzee Madiba kwa muda mrefu sasa ni pamoja na Zine El Abidine Ben Ali.
Huyu alikuwa Rais wa pili wa Tunisia, aliiongoza nchi hiyo katika kipindi cha mwaka 1987 hadi 2011. Kabla ya kushika wadhifa wa urais Ben Ali (74), aliteuliwa kuwa waziri mkuu Oktoba 1987 na Novemba 7 ya mwaka huo huo alishika wadhifa wa urais, baada ya kumwondo madarakani Rais Habib Bourguiba, mapinduzi yaliyotokea bila ya umwagaji damu.
Baadaye uchaguzi ulifanyika mwaka 1988, hatimaye kiongozi huyu alichaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo.
Hata hivyo, baada ya kukaa madarakani kwa muda mfupi, mwaka 2010 aliondolewa kutokana na maandamano makubwa yaliyofanyika nchini humo. Waandamanaji hao walikuwa wakihoji hali ya ukosefu wa ajira.
Januari 14 2011, Ben Ali na mke wake pamoja na familia yake waliikimbia nchi hiyo na kwenda kuishi uhamishoni nchini Saudia Arabia. Huku akiiacha nchi yake ikishikiliwa na Waziri Mkuu Mohamed Ghannouchi.
Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali zilizotolewa na vyombo vya habari hivi sasa rais huyo hajitambui, huku akipumua kwa mashine akiwa amelazwa katika Hospitali ya Jeddah nchini Saudi Arabia.


Hosni Mubarak
Muhammad Hosni Said Mubarak, maarufu kama Hosni Mubarak (85) alikuwa Rais wa Misri.
Aliongoza nchi hiyo katika wadhfa huo tangu 14 Oktoba 1981 hadi 11 Februari 2011.
Kabla ya kushika wadhifa wa urais mwaka 1975 aliteuliwa na Rais wa Misri Anwar as Sadat kuwa makamu wa Rais.
Sadat aliuawa mwaka 1981 na Waislamu wenye siasa kali hivyo Mubarak akawa Rais mpya. Januari 25, 2011 wananchi wa Misri waliandamana dhidi ya utawala wake na tarehe 11 Februari Mubarak alijiuzulu na kumkabidhi makamu wake madaraka yote.
Mwaka huohuo Mubarak alishtakiwa kwa mauaji ya waandamaji 800 wakati wa maandamano, pia ufisadi na wizi wa mali ya umma. Kabla ya kufikishwa mahakamani hali ya afya ya Mubarak iliripotiwa kuwa mbaya na baadaye Agosti 3,2011 alifikishwa kortini akiwa katika kitanda cha hospitali.
Tangu wakati huo amekuwa akiendelea na matibabu huku akiwa mahututi gerezani.
Ariel Sharon
Ariel Sharon Waziri mkuu wa 11 wa Israel ni miongoni wa viongozi walio kwenye hali ya kutokujitambua na kukata kauli ‘coma’.
Kwa muda wa miaka saba sasa kiongozi huyu amekuwa akipumulia mashine huku hali yake ikionekana kutokubadilika. Amekuwa katika hali hiyo tangu Januari 2006.
Mwaka huu vipimo vimeonyesha kuwa kuna hali ya kufanya kazi kwenye ubongo wake kulingana na picha na sauti zilizorekodiwa na wanafamilia wake.
Sharon alikuwa kamanda katika Jeshi la Israel tangu lilipoanzishwa mwaka 1948. Alianza kazi kama askari wa mwavuli na baadaye kuwa ofisa aliyeshiriki katika vita vya mwaka 1948 vilivyoikomboa Israel akiwa kiongozi wa platuni katika Brigadia ya Alexandroni.


Mbali na vita hiyo, ameshiriki pia vita vingi vikiwemo vya Ben Nun Alef. Alikuwa mtu muhimu katika uundwaji wa kikosi cha 101 kwa ajili ya kujibu mashambulizi.
Ameshiriki pia vita vya Suez vya mwaka 1956, vita vya siku sita vya mwaka 1967, vita vya mmomonyoko na vitav ya Yom-Kippur ya 1973.
Akiwa Waziri wa Ulinzi, aliongoza vita ya Lebanon mwaka 1982.
Akiwa bado jeshini, alijulikana kama kamanda mahiri katika historia ya Israel na mtu pekee mwenye mikakati ya kijeshi nchini humo.
Baada ya mashambulio katika vita ya Sinai katika vita ya siku sita na ile ya kulizunguka Jeshi la Misri katika vita ya Yom Kippur, wananchi wa Israel walimtungia jina na kumwita ‘Mfalme wa Israel’ na ‘Simba wa Mungu’.
Akiwa na upinzani mkali ndani ya Likud kutokana na sera yake hiyo, Novemba mwaka 2005 alijitoa kwenye chama hicho na kuunda Chama cha Kadima.
Ugonjwa wa kupooza ulimshika miezi michache akiwa mbioni kushinda katika uchaguzi, huku akielezwa kuwa na mpango wa kuiondoa Israel katika Ukanda wa Gaza.
Ronald Reagan
Ronald Regan alikuwa Rais wa 40 Marekani . Rais huyu alifariki mwaka 2004 baada ya kuwa kwenye koma akipumulia mashine kwa miaka 10 akiugua ugonjwa wa Alzheimer.
Kabla ya kuwa rais, Reagan alikuwa Gavana wa Jimbo la California kati ya mwaka 1967 hadi 1975 na mwigiza filamu wa redio (michezo ya radio).
Akiwa Rais, Regan alinusurika na jaribio la kupinduliwa na alikumbana na upinzani mkali kutoka vyama vya wafanyakazi na mapambano vya dawa za kulevya.
Alichaguliwa tena mwaka 1984 na kutangaza ‘Kumekucha Marekani’ huku akijihusisha zaidi na masuala ya uhusiano wa kimataifa ikiwa ni pamoja na kukabiliana na vita baridi dhidi ya Ukomunisti.
 Mwaka 1994, Reagan aligundulika kuwa na ugonjwa wa Alzheimer uliomweka hospitalini. Alifariki baada ya miaka 10 akiwa hospitalini.

No comments:

Post a Comment