CHEKA KWA RAHA ZAKO :

ZUZU alifika maskani akiwa amekasirika kupita kiasi. Rafiki yake Janja akamuuliza “Oya, vipi tena?”
ZUZU : Mke wangu ananidharau eti hajaona mwanamume mjinga kama mimi?
JANJA : Hajaona wajinga nini? Ngojanimwite yule dereva wa kibajaji ndio ujue duniani kuna wajinga.
JANJA akamuita dereva wa kibajaji na kumwambia “Oya, chukua hizi
shilingi elfu mbili, nenda nyumbani kwangu ukaniangalie kama nipo.”
Dereva wa kibajaji akachukua zile hela na kuongoka.
JANJA : “Umeona eeh? Sasa ujue kuna watu wajinga kaka! Huna haja ya kukasirika.
ZUZU akasema kwa masikitiko makubwa “Kweli yulemjinga sana, ningekuwa
mimi ningechukua hela na kukupigia simu tu nikuulize uko wapi?”
No comments:
Post a Comment