Thursday, 8 August 2013

WAINGEREZA WAMWAGIWA TINDIKALI

WAINGEREZA WAMWAGIWA 
TINDIKALI VISIWANI ZANZIBAR

Kama nalia vile
WAINGEREZA WAMWAGIWA TINDIKALI VISIWANI ZANZIBAR

Imeripotiwa kuwa wanawake wawili raia wa Uingereza wamemwagiwa tindikali katika eneo la mji mkongwe uliopo Unguja jana. 

Wanawake hao wenye umri wa miaka 18, ambao wamekuwa wanafanya kazi za kujitolea katika jamii visiwani humo, walimwagiwa tindikali usoni walipokuwa kwenye matembezi nyakati za jioni. Hata hivyo hadi sasa wahusika wa tukio hilo hawajakamatwa.

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi visiwani humo Mkadam Khamis amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema msako mkali wa kuwatafuta wahusika unaendelea.

Aidha taarifa zilizopatikana kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini zinasema “Serikali ya Uingereza imetoa tahadhari kwa watalii wanaopendelea kutembelea visiwa vya Unguja na Pemba kuhusu kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu dhidi ya wageni katika visiwa hivyo.”
Zanzibar

No comments:

Post a Comment