DK Bilali asema, mabadiliko
tabianchi bado tatizo Afrika
Arusha. Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal amesema
mabadiliko ya tabia ya nchi yameathiri kwa kiwango kikubwa makazi ya
watu wanaoishi maeneo ya mijini hasa katika nchi za Kiafrika, hivyo
juhudi za makusudi zinapaswa kuchukuliwa ili kukabiliana na athari hizo.
Akifungua mkutano wa kimataifa wa siku tatu jana
jijini Arusha, unaojadili changamoto ya ongezeko la kasi ya idadi ya
watu mijini na maendeleo Afrika unaosababishwa na mabadiliko ya
tabianchi alisema mkutano huo utatoa ufumbuzi ambao utafanyiwa kazi
kutokana miji mingi kuzalisha takataka kwa asilimia 80.
Dk Bilal alisema tangu kongamano la Habitat II
mwaka 1996 majadiliano juu ya idadi kubwa ya watu kuhamia mijini
imepitia kwenye mabadiliko mbalimbali, hivyo suala la mabadiliko ya
tabianchi kuendelea kuwa ni changamoto kubwa kimataifa.
No comments:
Post a Comment