SERIKALI inapata mapato ya takribani Sh. milioni 3.5 kwa siku kutokana na usafiri 
 wa treni katika jiji la Dares Salaam.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) Dk.Zacharia Mganilwa wakati akimkabidhi tuzo Waziri wa Uchukuzi, Dk.Harrison Mwakyembe kwa mchango wake mkubwa wa kuboresha sekta ya reli nchini kwa niaba ya kampuni ya Mwandi Tanzania kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Aidha Dk. Mganilwa tuzo pia imetolewa kutokana na  Waziri Mwakyembe 
ameweza kufufua na kuweka kwenye fikra Reli ya Musoma ya kwenda  Arusha 
na Reli Tanga.
Akizungumza katika makadhiano hayo,Dk.Mganilwa amesema  kuwa tuzo hiyo 
ilizingatia vigezo vyote muhimu vya  kumpata mshindi kwa kuzingatia 
mchango wa muhusika katika sekta ya  hiyo ,mtazamo wa wananchi kwa mtu 
husika na msimamo binafsi wa mtu husika kwenye uboreshaji  huo.
 “Ninyi ni mashuhuda wa mapinduzi ya usafiri wa treni za abiria jijini 
Dar es Salaam unaowanufaisha zaidi ya abiria 14,000 kila siku na 
ikumbukwe kwamba wazo la kuanzishwa usafiri huo lilikuwepo lakini 
Mheshimiwa Waziri ndiye aliyekuja  kufanya ndoto hiyo kuwa 
uhalisia”alisema Dkt.Mganilwa.
Tuzo hiyo imepatikana baada ya kushindanishwa kwa majina matatu ya watu 
ambao wana mchango mkubwa kwenye maendeleo na mapinduzi ya reli Tanzania
 kwa kurejea kila mmoja katika kipindi chake cha na kile alichokifanya.
Aidha ameiomba Serikali kupitia wizara ya hiyo kuanzisha mfuko wa miundo
 mbinu kwa fedha zitakazo kuwa zinapatikana katika usafirshaji ili 
kuweza kuendelea kuboresha suala hilo na  kukuza uchumi wa nchi yetu 
pamoja na kuleta maendeleo.
Naye Waziri Mwakyembe ameishukuru kampuni   hiyo kwa kuuona mchango wake
 katika jamii na kuweza kumpatia tuzo, ambayo  ni motisha   itakayo 
muongezea juhudi za kuliletea Taifa letu maendeleo kupitia sekta ya 
hiyo.
“Kwa niaba ya TRL, RHACO na wafanyakazi wote wa wizara ya Uchukuzi 
napenda kuishukuru kampuni  ya Mwandi Tanzania kwa kuuona mchango wangu 
katika sekta ya usafiri wa treni bado tunaendelea kuweka mipango 
madhubuti kuboresha usafiri wa treni nchini na Afrika Mashariki 
kiujumla”
 alisema Dkt.Mwakyembe.
 Watu  wengine walioshiriki katika ushindani wa tuzo hiyo, Injia Festo 
Mwanyika na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Reli  Tanzania na Linford 
Mboma kutoka   Shirika la Reli la Tanzania  na Zambia (TAZARA).
No comments:
Post a Comment