Polisi, Interpol wakamata
shehena ya mihadarati
JESHI la Polisi Nchini kupitia kitengo cha askari wake wa Interpol limekamata shehena ya dawa za kulevya, magari na silaha.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Kamishna Robert Manumba alisema operesheni hiyo ilifanyika kwa siku tatu (Julai 16 hadi 18 mwaka huu).
DCI Manumba |
Alisema katika operesheni hiyo magari 3348 yalikamatwa huku 32 yakikutwa na makosa ambapo 22 yaliibwa Japan (10), Uingereza (5), Malaysia (3), Tanzania (2) Afrika ya Kusini (1) na 10 yaligunduliwa kuingiliwa chassis zake.
Aliongeza kuwa katika operesheni hiyo wahamiaji haramu 305 walikamatwa nchini ambapo raia wa Burundi ni 230, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo (DRC) 30, ambao walikamatwa Kagera na Kigoma.
Wahamiaji haramu wengine kutoka Ethiopia (24) waliokamatiwa mkoa wa Pwani, Rwanda (15), Kenya (3) na Somalia (3).
Mkurugenzi huyo alisema operesheni hiyo ilikamata silaha haramu 28 ambazo ni Pistol (1), AK 47 (1), Short Gun (1), Rifle (3) Gobole (21) na risasi 24.
Makosa mengine waliokamata askari hao ni pamoja na meno ya Tembo vipande vinne, ngozi moja ya nyoka, box 7 za kalamu, katoni 40 za pombe kali aina ya cheers sprirt na pombe zilizokwisha muda wake.
No comments:
Post a Comment