Vitu vya kuzingatia  unapotaka kununua kompyuta 
Muongozo: Vitu vya kuzingatia
 unapotaka kununua kompyuta 

 
 
   
    
 kununua kompyuta iwe laptop au desktop huwachanganya watu wengi 
hasa wasiokuwa na uzoefu wa vifaa hivi maana ukifika dukani utakuta za 
kila namna na miundo tofauti, nimeona niandike makala hii kuwasaidia 
wale wanunuaji wapya wapate muongozo ili angalau wanapokwenda dukani 
wajue wanataka nini.
     kununua kompyuta iwe laptop au desktop huwachanganya watu wengi 
hasa wasiokuwa na uzoefu wa vifaa hivi maana ukifika dukani utakuta za 
kila namna na miundo tofauti, nimeona niandike makala hii kuwasaidia 
wale wanunuaji wapya wapate muongozo ili angalau wanapokwenda dukani 
wajue wanataka nini.
10. Matumizi
unapotaka kununua kompyuta, jambo la kwanza ni kujua unataka kwa ajili 
ya matumizi yapi? kuna watumiaji ambao wao ni kufungua facebook, kusoma 
barua pepe tu na kutype kazi zake ndogo ndogo hawa wanahitaji pc zisizo 
na specification kuubwa, kuna ambao wanafanya photoshoping, video 
editing hawa wanahitaji mashine zenye option kubwa za multimedia.

9.
Bei
hapa ndo uwa patamu maana, utakuta mtu anataka kompyuta yenye 
specification kuubwa mfano ram Gb 6, au processor quad core, hard disk 
 GB kuendelea halafu anakwambia ana laki sita, kama huna hela ya 
kutosha sio tatizo, unaeza ku upgrade kidogo kidogo baadae ukipata hela,
 mfano nunua ram gb1 then baadae utaongeza mpaka zifike hata 6 kama 
mashine inaruhusu, au hard disk kama ni ndogo unaweza nunua kisha siku 
za baadae ukaongeza.

8.Operating System
angalia minimum requirement ya hiyo kompyuta unayonunua, mara nyingi uwa
 imeoneshwa kuwa hiyo pc imedesgniwa kwa ajili ya operating system gani,
 zipo kwa ajili ya ubuntu, zipo windows xp, 7, 8 etc
7. Ukubwa wa umbo
baadhi ya watu kama mimi napenda skrini kubwa kama desktop haina kuanzia
 inch 22 au laptop ianzie inc 15 uwa sina raha maana mimi ni mpenzi wa 
movies na games, jambo la muhimu ni kuwa skirini kubwa ni nzuri kwa wale
 wenye macho yenye udhaifu. ila kuna ambao wanapenda vile vidogo vidogo 
labda kwa sababu ni rahisi kubeba nakadhalika.

6. Matundu
kutokana na mahitaji yako, angalia kompyuta ambayo itafaa ukiwa umeweka 
flash pia unaweza kuweka modem, printer nakadhalika, siku hizi kuna hdmi
 connection, kuna usb 2 na usb 3 ports, matundu ya internet connection

5. jina
baadhi ya watu kwa sababu moja au nyingine atakwambia amnapenda HP au 
Dell au Samsung au Toshiba, mfano unaponunua pc ya Hp au samsung unapewa
 warant ikizingia unaweza irudisha ukatengenezewa au ukapewa mpya, 

4. Hard Disk
kwa watumiaji wa kawaida sio tatiuzo sana hii, ila kwa watumiaji 
wakubwa{wale wanopenda kudownload softwares mfano adobe suit uwa zina 
mpaka 5GB} wale wapenzi wa kudownload movies,  gaming , na wengineo 
wanahitaji hard disk kubwa. Magwiji wa komyuta huulizia SATA au SCSI 
drives

3. RAM
kwa watumiaji wadogo sio ishu sana hii, hata ram ya 2Gb ni kubwa kutosha
 matumizi ytake yoote. ila watumiaji wakubwa hasa wale professionals 
wangependa kutumia kuanzia 4 - 6 GB. pia operating systems kama windows 
32bit na 64bit zina minimum requirements za Ram itakayotumika 
kuziendesha.wataalam wa komyuta wenyewe wakati wa manunuzi huulizia DDR2
 au DDR3

2. Processor
kuna tofauti kubwa sana kati ya processor za single core kama pentium processors, duo-core, na quad core processors, 
kwa mtumiaji wa kawaida pc yenye processor za intel i3 inamtosha saaana
watumiaji wa kati i5 itafaaa ila kwa wale maguru i7 ndio ya kwao

1. Waranti
Kama utanunua kifaa chako kutoka katika maduka au mawakala wa icho kifaa
 wanaofahamika utapata waranti ambayo itasaidia wewe mtumiaji kupata 
msaada kifaa kitakapopata matatizo mfano battery ikizingua 
kamahujaiharibu mwenyewe unaweza kubadilishiwa ukapewa ingine 
nakadhalika

kwa leo tuishie hapa, kama umepata chochote hapa, Gonga Like, maswali, michango mingine yoyote inakaribishwa
addictiveTips
 
 
 
 
 
          
      
 
  
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment