Monday, 26 August 2013

DR. KINGWANGALLAH aagiza....

 
 
 
 
DR. KINGWANGALLAH : NILETEENI MAJINA YA 
WAUZA UNGA NIKAYATAJE BUNGENI
 
  Mbunge wa Nzega kupitia CCM, Dr. Hamisi Kingwangallah ameitosa kusaidiana na Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa CCM, Dr.
Harrison Mwakyembe, katika vita vya kupambana na wauzaji wa dawa za kulevya nchini.

Akizungumza jana, Dr. Kingwangallah alimpongeza Waziri Mwakyembe na kuitaka Serikali, Bunge na Mahakama kumuunga mkono kwani vita hii ni yetu sote. Kwa upande wake amewaomba wananchi wenye taarifa na ushahidi usio na mashaka ikiwa ni pamoja na majina ya wazungu wa unga kumpelekea ili akayataje Bungeni kwenye mkutano wa 11 unaoanza mjini Dodoma tarehe 27 Agosti.

Katika kuthibitisha dhamira yake, pia amesambaza taarifa hizi kupitia mitandao kadhaa ya kijamii ikiwamo ukurasa wake wa Facebook. Dr. Kingwangallah amesema hadi sasa ana majina saba na amekwishamwandikia barua Spika wa Bunge, Mheshimiwa Anne Makinda, kuomba fursa ya kuwataja wahusika wa dawa za kulevya kwa mujibu wa taarifa atakazopokea.
sembe...au Unga

CCM, Dr. Hamisi Kingwangallah

 
(kwa habari zaidi tembelea )
(http://www.dar24.com/)
 
 

simba mawindoni
 

No comments:

Post a Comment