ITAKUWA KAMA NDOTO SIKU YA KUFA KWANGU.
Itakuwa kama ndoto pale moyo wangu utakapozima kama mshumaa uliopulizwa
na upepo. Utatamani niamke angalau usikie sauti yangu, lakini tayari
utakuwa
umeshachelewa......kilio, huzuni, simanzi na majonzi vitakuwa
vimetanda katika kuta za moyo wako....machozi yatakutoka kila
utakapokumbuka; Ucheshi wangu na moyo utakuwa mpweke kila utakapoiona
namba yangu kwenye simu yako. Utatamani uifute ila roho
"itakuuma sana
kwa kuwa umenizoea sana."
- Hivyo jaribu kufurahia uwepo wangu kabla
sijatoeka duniani.......kwani chura anajua umuhimu wa maji baada ya maji
kukauka. Tupendane jamani, maisha yenyewe ya hapa duniani ni mafupi
sana.
No comments:
Post a Comment