- WACHUNGAJI WA DECI WAHUKUMIWA
- WALIOPANDA MBEGU KURUDISHIWA
|
Wana maombi |
|
- WACHUNGAJI WA DECI WAHUKUMIWA |
Vigogo wanne wa iliyokuwa Kampuni ya Development Entrepreneurship for
Community Initiative (DECI) wamehukumiwa kwenda jela miaka mitatu au
kulipa faini ya sh milioni 21 kila mmoja.
|
Wana maombi |
Hukumu hiyo ilitokewa na Hakimu Mkazi Alocye Katemana wa Mahakama ya
Kisutu, Dar es Salaam. Aidha, Mahakama imeagiza kuwa pamoja na adhabu
hiyo Serikali ifanye mchanganuo wa mali za DECI ambazo inazishikilia,
kwa kuwa zipo mali zilishikiliwa zisizo za kampuni hiyo bali za watu
wengine.
Alisema kuwa fedha za wateja wa DECI walizopanda
zirejeshwe kwa wateja wenyewe ambao wataonesha uthibitisho wa kweli kuwa
walipanda fedha zao huko.
Katika hukumu hiyo iliyotolewa na
Hakimu Mkazi, Stewart Sanga na kusomwa na Hakimu Katemana, washitakiwa
walikuwa watano, ambao ni Jackson Mtares, Dominick Kigendi, Timotheo ole
Loitginye, Samwel Mtares na Arbogast Kipilima. Hata hivyo Arbogast
Kipilima aliachiliwa huru baada ya Mahakama kutokumpata na hatia.
Washitakiwa hao walikuwa wanatetewa na mawakili wa kujitegemea Hudson Ndusyepo na Onesmo Kyauke.
Wakili Mwangamila alidai washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka
mawili ambayo ni kuendesha na kusimamia mradi wa upatu kinyume cha
kifungu 111A (1,3) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16.
Alidai kuwa, kati ya mwaka 2007 na Machi 2009, katika makao makuu ya
DECI , yaliyopo Mabibo Mwisho, jijini Dar es Salaam, washitakiwa
waliendesha na kusimamia mradi wa upatu katika sehemu tofauti nchini,
kwa ahadi ya kuwapa wanachama wao fedha zaidi ambazo katika mazingira ya
kibiashara ni kubwa kuliko mradi waliokuwa wakiufanya.
Mwangamila alidai kuwa, shitaka la pili ni kupokea amana za umma bila
kuwa na leseni, kinyume cha kifungu cha 6 (1,2) cha Sheria ya mabenki na
Taasisi za Fedha Na. 5 ya mwaka 2006 na kwamba, washitakiwa wote katika
kipindi hicho wakiwa kwenye ofisi zao za DECI , walipokea amana kutoka
kwa umma bila leseni.
|
Zigua simo na njero |
No comments:
Post a Comment