Bodaboda ni janga,
Serikali Hili
Katika siku za hivi karibuni kumeibuka tabia ya waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda kujichukulia sheria mkononi pindi kunapotokea ajali zinazohusisha magari na pikipiki.
![]() |
| wazi hilo |
![]() |
| elimu kutolewa |
Mara tu ajali inapotokea, huanza kupigiana simu na
kuitana na baada ya dakika chache utakuta kundi kubwa la waendesha
bodaboda hao wamezingira gari na kuanza kujichukulia sheria mkononi.
Vijana hao badala ya kutoa taarifa polisi ili
wafike na kufanya kazi yao, wao ndiyo hugeuka polisi na kuingia mitaani
kumsaka aliyesababisha ajali iwapo anakuwa ametoweka kunusuru maisha
yake.
Wanapomkuta “mhalifu”, badala ya kumpeleka polisi wao wanaamua kumsulubu kana kwamba wao wako juu ya sheria.
Kwenye gari lililohusika kwenye ajali, baadhi yao
huvunja vioo, wengine hutembezea kipigo kwa dereva na hata abiria
wasiohusika, kuiba mali za waliokuwepo kwenye gari husika na mara kadhaa
imetokea hata kuchoma moto magari.
Tabia hii ikiachwa izoeleke kwamba bodaboda wajichukulie sheria mkononi, hakika tutakuwa tunatengeneza bomu la hatari.
Tayari kumeanza kujitokeza uhasama kati ya
madereva wa magari na bodaboda kiasi kwamba wamiliki wa magari sasa
hawataki kutoa msaada kwa waendesha bodaboda wanapopata ajali.
Nimeshuhudia mmoja amegongwa na kila gari lililokuwa linapita eneo la ajali dereva akiombwa msaada, utasikia “hao wamezidi”.
Asilimia 95 ya ajali zote zinazotokea nchini
zikihusisha pikipiki, chanzo cha ajali hizo mara nyingi kinakuwa ni
wenyewe waendesha pikipiki. Huu ndiyo ukweli, kwamba sasa hili ni janga
la kitaifa.
Ni jambo la kawaida mwendesha bodaboda kulipita
gari kupitia upande wa kushoto na wakati mwingine dereva wa gari
ameshaonyesha ishara kuwa anakata upande wa kushoto. Wakati mwingine
pikipiki mbili hulipita gari kwa wakati mmoja, kila moja ikipita upande
wake.
Na si ajabu kukuta mwendesha bodaboda anawasha taa
akionyesha ishara kuwa anakata kulia, lakini akakata kushoto au kinyume
chake.
Katika siku za hivi karibuni kumeibuka tabia ya waendesha
pikipiki maarufu kama bodaboda kujichukulia sheria mkononi pindi
kunapotokea ajali zinazohusisha magari na pikipiki.
Bila kujali ni nani mwenye makosa katika ajali
hizi, waendesha pikipiki hao wameanzisha mtandao wa kuwashambulia
madereva wa magari yanayohusika katika ajali hata kama wao ndio wenye
makosa.
Mara tu ajali inapotokea, huanza kupigiana simu na
kuitana na baada ya dakika chache utakuta kundi kubwa la waendesha
bodaboda hao wamezingira gari na kuanza kujichukulia sheria mkononi.
Vijana hao badala ya kutoa taarifa polisi ili
wafike na kufanya kazi yao, wao ndiyo hugeuka polisi na kuingia mitaani
kumsaka aliyesababisha ajali iwapo anakuwa ametoweka kunusuru maisha
yake.
Wanapomkuta “mhalifu”, badala ya kumpeleka polisi wao wanaamua kumsulubu kana kwamba wao wako juu ya sheria.
Kwenye gari lililohusika kwenye ajali, baadhi yao
huvunja vioo, wengine hutembezea kipigo kwa dereva na hata abiria
wasiohusika, kuiba mali za waliokuwepo kwenye gari husika na mara kadhaa
imetokea hata kuchoma moto magari.
Tabia hii ikiachwa izoeleke kwamba bodaboda wajichukulie sheria mkononi, hakika tutakuwa tunatengeneza bomu la hatari.
Tayari kumeanza kujitokeza uhasama kati ya
madereva wa magari na bodaboda kiasi kwamba wamiliki wa magari sasa
hawataki kutoa msaada kwa waendesha bodaboda wanapopata ajali.
Nimeshuhudia mmoja amegongwa na kila gari lililokuwa linapita eneo la ajali dereva akiombwa msaada, utasikia “hao wamezidi”.
Asilimia 95 ya ajali zote zinazotokea nchini
zikihusisha pikipiki, chanzo cha ajali hizo mara nyingi kinakuwa ni
wenyewe waendesha pikipiki. Huu ndiyo ukweli, kwamba sasa hili ni janga
la kitaifa.
Ni jambo la kawaida mwendesha bodaboda kulipita
gari kupitia upande wa kushoto na wakati mwingine dereva wa gari
ameshaonyesha ishara kuwa anakata upande wa kushoto. Wakati mwingine
pikipiki mbili hulipita gari kwa wakati mmoja, kila moja ikipita upande
wake.
Na si ajabu kukuta mwendesha bodaboda anawasha taa
akionyesha ishara kuwa anakata kulia, lakini akakata kushoto au kinyume
chake.

No comments:
Post a Comment