Friday, 23 August 2013




Wafugaji waliovamia Wilayani

 Handeni watakiwa kuondoka




Handeni. Wafugaji walioingia kinyemela katika Wilaya ya Handeni Tanga, wametakiwa kuondoka ndani ya wiki mbili, la sivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Agizo hilo lilitolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu katika mkutano uliofanyika Kata ya Kwamatuku Kitongoji cha Kwabalanga baada ya baadhi ya wanakijiji wa eneo hilo kutaka kauli ya serikali juu ya wimbi la wafugaji hao..
Diwani wa Kata ya Kwamatuku, Mustafa Beleko alimweleza Mkuu wa Wilaya kuwa kata yake imevamiwa na wafugaji ambao wameleta mifugo bila utaratibu stahiki.

No comments:

Post a Comment