CHA KALE DHAHABU |
SHUJAA WA MZIKI..TZ |
rasmi jukwaa la muziki huo kwa kufanyiwa tamasha maalumu la kumuaga, baada ya kudumu kwa takriban miaka 53 akiimba.
Tamasha hilo lilifanyika Ukumbi wa TTC uliopo
Chang’ombe wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam, ambapo pamoja na
kujitokeza matatizo ya kiufundi yaliyosababisha kuchelewa kuanza kwake,
tamasha hilo lilikuwa na kila aina ya mambo ya kuvutia na kuwaridhisha
mashabiki waliofurika kwenye viwanja hivyo.
Pazia la kuagana lafunguliwa
Saa nne usiku, Bendi ya Talent inayoongozwa na
mwanamuziki mkongwe, Hussein Jumbe ilifungua jukwaa kwa kuimba wimbo
wake wa ‘Pombe nimeikosea heshima’, ulioamsha shangwe za mashabiki
waliopamba ukumbi huo.
Wasifu wa Gurumo wawanyamazisha mashabiki
Katika tukio lilivuta zaidi hisia za mashabiki
waliotulia kimya wakisikiliza ni wasifu wa mwanamuziki Gurumo uliosomwa
na mchambuzi wa muziki Rajabu Zomboko, ambaye pamoja na mambo mengine
alieleza maisha ya muziki ya nguli huyo bila kuacha jambo lolote.
Zomboko aliwaduwaza mashabiki alipoeleza kwamba
tangu alipoanza muziki rasmi mwaka 1963, Gurumo hajawahi kupumzika
kupanda jukwaani, mbali na kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo
bendi nyingi huwa mapumzikoni.
Gurumo atangaza warithi wa kazi zake
Katika hali ya kawaida ni jambo gumu kukubali kazi
za wengine na kujilinganisha nao hata katika muziki, lakini kwa Gurumo
hilo halikuwa hivyo, bali alimtaja Hussein Jumbe kuwa ndiye chaguo lake
la kwanza kwa wanamuziki wanaoweza kurithi mikoba yake.
Gurumo alifanya hivyo huku akieleza kuwa anaamini
Jumbe anaweza kuyafanya aliyoyafanya yeye akiwa jukwaani ambapo alisema:
“Huyu ni chaguo langu la kwanza, atarithi mikoba yangu. Ninamkabidhi
maiki hii kama ishara ya kukubali anachokifanya na nina imani atadumu
kwenye muziki kama mimi.”
Mkongwe huyo alitoa maneno hayo kisha kumkabidhi
kipaza sauti Jumbe, ambaye aliimba wimbo wa Gama uliotungwa na Cosmas
Chidumule alipokuwa na Bendi ya DDC Mlimani Park enzi hizo huku akimtaja
mwanamuziki Edo Sanga kuwa ni chaguo lake la pili na chaguo lake la
tatu lilikuwa ni Juma Katundu.
Alisema kuwa hataki muziki wa dansi ufe, bali
uendelezwe na kwamba ndiyo sababu ya yeye kuwachagua wanamuziki vijana
na wenye bidii ili wafanye kazi kama aliyofanya yeye kabla ya kuamua
kustaafu.
BONYEZA HAPA....UJIPATIE HABARI.
1
|
2BONYEZA HAPA....UJIPATIE HABARI.
SIMBA DUME |
No comments:
Post a Comment