KITENGO CHA MAHELA....watu wataka kutoana vishipa..hahahahhaaahha!
KITENGO CHA MAHELA

Leo
nimesoma kuwa Kitengo cha Fedha chatoa tamko kuhusu kodi ya
laini ya simu aka sim card tax :
"amewataka watumiaji wa mitandao ya
simu nchini na watanzania kwa ujumla kuwa na subira kuhusu tozo ya Sh
1,000 kwa mwezi ..Alisema serikali inaendelea kupokea maoni kuhusiana na
suala hilo .. tangu itolewe kauli hiyo yamekuwapo manung’uniko mengi
kutoka kwa watu mbalimbali wakiwamo watumiaji wa mitandao ya simu"
Sasa mi naomba tafadhali kama mwananchi na mpiga kura, viongozi wetu
WASITUTANIE .. kodi au tozo hii kandamizi ilitungiwa kipengele katika
sheria na ilipitishwa tena kinyemela bungeni.. sasa maoni wanachukua ya
nini??!! Basi wasubiri mpaka warudi bungeni tutawapelekea salamu zao.
Ndugu zangu... wasituchanganye na tamko hili za kukinzana/kutuchanganya .........tetetetetetetetetete!!!!!!!!!!
No comments:
Post a Comment