Mfumuko wa bei
taifa wapungua
Dar es Salaam. Ofisi ya Takwimu ya Taifa
(NBS),imesema mfumuko wa bei wa taifa kwa Juni,mwaka huu,umepungua hadi
kufikia asilimia 7.6 kutoka asilimia 8.3 ya Mei Mwaka huu.
Mkurugenzi wa Takwimu wa NBS,Albina Chuwa amesema
uwezo wa Sh100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umepungua
hadi Sh71 na senti 43,Juni, 2013 kutoka Septemba,2010.

Chuwa alisema kuwa mfuko wa bei za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula ,umepungua hadi asilimia 7.4 Juni,mwaka huu kutoka asilimia 7.7 kwa Mei mwaka huu.
“Badiliko la bei za bidhaa zisizo za vyakula limepungua hadi asilimia 7.9 Juni,mwaka huu ukilinganisha na asilimia 9.2 Mei mwaka huu,”
alisema .
Alisema mfumuko wa bei ambao haujumuishi vyakula
na nishati kwa Juni mwaka huu,umepungua hadi asilimia 6.6 ikilinganisha
na asilimia 7.1 Mei.
Pia alifafanua kuwa mfumuko wa bei ya nishati kwa Juni ,umepungua hadi kufikia asilimia 14.8 ikilinganisha na asilimia 20.1 Mei.
Tanzania ni miongoni mwa nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki inayoathiriwa na mfumuko wa bei mara kwa mara kutokana na
kuyumba kwa sarafu yake dhidi ya fedha za kigeni na uhaba wa bidhaa za
ndani kwenda nje.
No comments:
Post a Comment