-
jamani hakuna mtu wa kumpa
medali huyu jamaaa!!!
Kuna jamaa alikuwa anaishi karibu
na makaburi. Basi akajigundulia njia
ya kupata usafiri bila ya kulipa...
Akawa kila akikodi bodaboda au
bajaji mida ya jioni jioni alikuwa
anaomba kuachwa makaburini.....
Katikati ya safari akawa anajipaka
poda usoni na kuweka pamba
kwenye pua zake then wakati wa
kushuka anaongea kwa kubana
pua...
.
"Nimefika home unanidai shilingi
ngapi?!?"
.Madereva wote wa bodaboda na
bajaji walikuwa wanatoka nduki....
Siku moja akafanya mchezo huo
kwa dereva mmoja wa bodaboda
mtoto wa TANDALE kapinda
mbaya!!! Walipofika mwisho wa
safari dereva wa bodaboda
hakutishika na mapoda wala pamba
puani....
Akakomaa anataka nauli
yake!!!!
JAMAA: "Ooooooky!!!! Twende
kwenye kaburi langu nikakupe
chako....!!!"
Dereva ya boda boda kumbe
alikuwa ameshaskia story za jamaa
so akakomaa na kumwambia...
BAJAJI: "Haina noma mtu wangu....
Twende ukanipe changu nsepe...."
maana hasira nilizonazo naweza kukulamba wewe na mapoda yako
Walipofika kaburi fulani, jamaa
akagonga msalaba....
JAMAA: "Wakulu, wakulu fungueni
nipeni alfu nane huyu jamaa
ananidai nauli......!!!!"
Ghafla mkono mrefu wenye
manyoya ukatoka kaburini ukiwa
umeshika noti ya msimbazi....
DAAAH, NDUGU ZANGU ASUBUHI
KULIKUTWA PEA MBILI TUU ZA VIATU
KANDO YA KABURI, NA KIBAJAJI
!!!!!
Thursday, 18 July 2013
mtoto wa TANDALE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment