Ni dalili ya afya au ugonjwa?
Katika baadhi ya jamii zetu nyingi hasa kutoka bara la Afrika,
kumejengeka dhana kuwa kitambi /unene huashiria utajiri. Mila, imani na
desturi hii kwa kiasi fulani huchangia watu kutozingatia kanuni na
taratibu za lishe bora, pengine hii inatokana na mwamko mdogo wa elimu
ya afya jamii.

Wakati hali ikiwa hivyo miongoni mwa watu toka
bara letu la Afrika, kwa upande wa nchi zilizoendelea, watu huamini kuwa
unene/kitambi ni dalili tosha ya ugonjwa. Siyo hivyo tu bali pia
historia ya magonjwa katika fani ya elimu afya jamii inatueleza hivyo.
Kuna unene wa aina kuu mbili, kwanza ni ule unaosababishwa na
kutozingatia kanuni na taratibu za lishe bora / balance diet. Kwa mfano
ulaji wa vyakula vyenye kiasi kikubwa cha mafuta na wanga, unywaji wa
mara kwa mara wa pombe kama vile bia pamoja na kutofanya mazoezi ya
mwili na viungo. Aina ya pili ya unene ni ule unaotokana na urithi japo
kwenye mada hii msisitizo zaidi ni kwenye aina ya kwanza ya unene.
Kuna matatizo mbali mbali yanayo ambatana na unene/kitambi. Mosi,
madhara ya kiafya kama vile ugonjwa wa moyo, shinikizo la damu, kisukari
aina ya pili /diabetes type II. Pili, madhara ya kisaikolojia, hasa
pale mtu anapojishuku kupoteza mvuto/ aesthetic beauty. Hali imeshamiri
sana hasa katika nchi zilizoendelea ambapo watu huchukulia unene/kitambi
kama ulemavu fulani wa kimwili.
Pamoja na hayo, wakati
mwingine tunafanya makosa kuwahukumu binadamu kulingana na mwonekano wa
maumbile yao, kwani hakuna hata moja kati yetu anaweza kuingilia kazi ya
uumbaji, ninasema hivi kwasababu hatuwezi kujua ni nini chanzo hasa
ambacho kinapelekea mtu kuwa mnene au kuwa na kitambi. Kama nilivyosema
awali, kuna aina ya unene/kitambi kinachotokana au kusababishwa na
urithi.
Namna ya kukabiliana na matatizo yatokanayo na
unene/kitambi, wakati watu katika mataifa yanayoendelea, hujikita zaidi
kwenye matumizi ya magari hasa magari binafsi, kidogo hali ni tofauti
katika nchi zilizoendelea ambapo msisizito kwao ni kwenaye matumizi ya
usafiri wa umma, matumizi ya baiskeli na hata matembezi ya miguu kwa
sehemu zinazofikika. Kwa hili wenzetu wa mataifa yaliyoendelea
wamefanikiwa vya kutosha kwa kuwekeza na kutenganisha barabara za magari
na zile za waendesha baiskeli na watembea kwa miguu.
Mwisho,
njia pekee ya kukabiliana na changamoto hii ya unene/kitambi, ni kwa
kuzingitia kanuni za lishe bora kwa kujisomea majarida yanayohusu elimu
ya afya kwa jamii na kujijengea tabia ya kufanya mazoezi ya mwili na
viungo. Muhimu kuliko yote, kama itawezekana ni kupunguza ulaji wa nyama
choma na unywaji wa bia wa mara kwa mara.
Ni dalili ya afya au ugonjwa?
Katika baadhi ya jamii zetu nyingi hasa kutoka bara la Afrika, kumejengeka dhana kuwa kitambi /unene huashiria utajiri. Mila, imani na desturi hii kwa kiasi fulani huchangia watu kutozingatia kanuni na taratibu za lishe bora, pengine hii inatokana na mwamko mdogo wa elimu ya afya jamii.
Kuna unene wa aina kuu mbili, kwanza ni ule unaosababishwa na kutozingatia kanuni na taratibu za lishe bora / balance diet. Kwa mfano ulaji wa vyakula vyenye kiasi kikubwa cha mafuta na wanga, unywaji wa mara kwa mara wa pombe kama vile bia pamoja na kutofanya mazoezi ya mwili na viungo. Aina ya pili ya unene ni ule unaotokana na urithi japo kwenye mada hii msisitizo zaidi ni kwenye aina ya kwanza ya unene.
Kuna matatizo mbali mbali yanayo ambatana na unene/kitambi. Mosi, madhara ya kiafya kama vile ugonjwa wa moyo, shinikizo la damu, kisukari aina ya pili /diabetes type II. Pili, madhara ya kisaikolojia, hasa pale mtu anapojishuku kupoteza mvuto/ aesthetic beauty. Hali imeshamiri sana hasa katika nchi zilizoendelea ambapo watu huchukulia unene/kitambi kama ulemavu fulani wa kimwili.
Pamoja na hayo, wakati mwingine tunafanya makosa kuwahukumu binadamu kulingana na mwonekano wa maumbile yao, kwani hakuna hata moja kati yetu anaweza kuingilia kazi ya uumbaji, ninasema hivi kwasababu hatuwezi kujua ni nini chanzo hasa ambacho kinapelekea mtu kuwa mnene au kuwa na kitambi. Kama nilivyosema awali, kuna aina ya unene/kitambi kinachotokana au kusababishwa na urithi.
Namna ya kukabiliana na matatizo yatokanayo na unene/kitambi, wakati watu katika mataifa yanayoendelea, hujikita zaidi kwenye matumizi ya magari hasa magari binafsi, kidogo hali ni tofauti katika nchi zilizoendelea ambapo msisizito kwao ni kwenaye matumizi ya usafiri wa umma, matumizi ya baiskeli na hata matembezi ya miguu kwa sehemu zinazofikika. Kwa hili wenzetu wa mataifa yaliyoendelea wamefanikiwa vya kutosha kwa kuwekeza na kutenganisha barabara za magari na zile za waendesha baiskeli na watembea kwa miguu.
Mwisho, njia pekee ya kukabiliana na changamoto hii ya unene/kitambi, ni kwa kuzingitia kanuni za lishe bora kwa kujisomea majarida yanayohusu elimu ya afya kwa jamii na kujijengea tabia ya kufanya mazoezi ya mwili na viungo. Muhimu kuliko yote, kama itawezekana ni kupunguza ulaji wa nyama choma na unywaji wa bia wa mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment