Umesahau nini kwa
mpenzi wako wa zamani?
![]() |
mniache nicheke nisije nikapasuka |
mpendwa, huku nikiamini kuwa tutaendelea kuwa pamoja siku
ya leo, kama ilivyokuwa kawaida yetu ya kukutana kwenye kona hii kujadili mambo
mbalimbali ya uhusiano na maisha.
Raha kwenda mbele
Nakushukuru
kama wewe ni miongoni mwa
![]() |
Tafadahali mama tusahau vya taraka |
Ndugu
msomaji wangu mpendwa, kuna vitendo vinavyoumiza kichwa, hivi ni kuona baadhi
ya watu wanajenga ukaribu wa kupitiliza kwa wapenzi wao wa zamani kiasi cha
kuzua hofu kwa wenzi wao.
Ukiacha
wale waliopata mtoto katika kipindi cha uhusiano, au wanandoa walioachana huku
wakiwa na mtoto, hao wanaruhusiwa kuwasiliana mara kwa mara kulea mtoto. Ubaya
upo kwa wale walioachana, lakini muda wote wapo katika mawasiliano makubwa,
huku wakiwa hawana chochote kinachowaunganisha.
Wakati
mwingine hualikana chakula cha mchana au usiku, muda mwingine huchukuana na
kwenda katika majumba ya starehe, kama vile bado wapo kwenye mapenzi kama
ilivyokuwa awali.
Hii ni
mbaya sana,
maana kama mlishaachana huo ukaribu uliojenga kwa sasa ni ishara
gani?
![]() |
haba na haba huleta mahaba |
Je, huoni
sasa ni wakati wako kurudiana na huyo mpenzi wako wa zamani, ili kumuondolea
jakamoyo mpenzi wako mpya? Haya ni maswali ambayo tunapaswa kujiuliza kila
mara.
Kuna
baadhi ya watu ambao baada ya kuachana na wapenzi wao wa zamani, hushindwa
kujizuia na kutafuta mahala kwa kujiegemeza, ili watulize majonzi ya kuachwa.
Kwa
bahati nzuri wakapata watu wanaowapenda kwa dhati, ambao wamekuwa wakiwajali
kwa kila wanachokitaka katika suala zima la mapenzi wanayoyapata, wanatembea
kifua mbele wakithaminiwa na wapenzi wao wapya.
Lakini
kutokana na ujinga, anajikuta anaingia tena katika urafiki na yule aliyeachana
naye kipindi cha nyuma, sasa unabaki unashangaa chanzo na mwelekeo wake.
Si kila
mtu anahitaji kuona mchumba wake aliyekuwa naye ana ukaribu na mpenzi wake wa
zamani, hakuna anayependa suala hilo. Ni wazi wapenzi wa zamani wanapokuwa na
ukaribu wa kupitiliza, suala la ngono kwao ni lazima.
Kama
watafanya ngono,
si kweli kama wataogopana kiasi cha kuweza kujikinga katika
suala hilo, zaidi wataingiliana kimwili bila tahadhari yoyote, matokeo yake ni
kupeana maradhi.
Hapo
ndipo utakuta cheni kubwa ya maambukizi, kwani wakishaambukizana maradhi
huwapelekea wapenzi wao hao wapya, ukiwa ni mtindo usiokuwa na mashiko hata
kidogo. Ni jukumu letu kujua hakuna ulazima wa kudumisha ukaribu na wapenzi
wetu wa zamani.
Watu
wabakie kulea watoto, kama katika hatua ya mapenzi yao walibahatika kupata
zawadi hizo kutoka kwa Mungu. Na kama unaona kuna ulazima wa kuwa na ukaribu na
mtu wako wa zamani, basi jaribuni kuzungumza namna ya kurudiana, ili usilete
mkanganyiko kwa wengine.
Kuachana
kupo, lakini pia kurudiana si jambo geni duniani, ukiona huwezi kukaa bila
kumuona mpenzi wako wa zamani, kumpigia simu au kuwasiliana naye muda wowote,
mpigie magoti mrudiane.
Kinyume
na hapo,
utasababisha maswali mengi kutoka ndani ya moyo wako na jamii kwa
ujumla, utampa presha uliyekuwa naye, maana anaona ujinga wako, kimekushinda
mwenyewe mwanzo na sasa unajirudisha kienyeji.
Katika
jamii wapo watu wengi wenye tabia hizo, wanaachana na wapenzi wao lakini muda
wote wapo pamoja. Baadaye wanaanzisha tena uhusiano na kuendelea na uchafu wao.
Wanasababisha
presha kwa wengine, hivyo hakuna haja ya kujinyima kama kweli waliachana kwa
bahati mbaya, basi rudisheni tena penzi lenu ili watu wajue moja, kuliko
kusumbua wenzenu.
Huo ndio
ukweli, maana wengi wamekuwa wakiwaza na kuumiza kichwa kuona waliokuwa nao,
wana ukaribu wa kupitiliza na wapenzi wao wa zamani, hivyo kuwachanganya
kisaikolojia.
Nimeandika
makala haya kama majibu ya baadhi ya wasomaji wangu, waliohoji uhalali wa
wapenzi wao, wachumba wao kuwa na ukaribu na wapenzi wa zamani, tena wengineo
wakiandikiana hadi meseji za mapenzi.
Hii sio
haki na kuna ulazima wa jamii, kutambua huo ni mpango mbaya na unaweza
kudhalilisha watu wengine.
No comments:
Post a Comment