Wednesday, 4 September 2013

UKITAKA CHEKA KUNUNA SI HAKI YAKO...

 
 
 
UKITAKA CHEKA KUNUNA SI HAKI YAKO...
CHEKA
Duuuuuu!

Siku moja mtoto wakike mwenye umri wa miaka 11 alimuuliza baba yake, “baba utanipa zawadi gani katika siku yangu ya kuzaliwa nikifikisha miaka 15?”

Baba alimjiu kwa kifupi, “Bado muda upo wa kutosha nitakuandalia zawadi.”

Yule binti akiwa na umri wa miaka 14 alianguka ghafla na kukimbizwa hospital.

Madaktari wakamchunguza na kusema tatizo lake lilikuwa ni moyo na kwa vyoyote vile kwa jinsi moyo wake ulivyo angekufa.

Baba alikuwa karibu yake pale kitandani na binti akauliza:

“Baba,. Wamekuambia kuwa nitakufa ?”

Baba akajibu mwanangu hutakufa utaishi na akafuta machozi yake.

Mtoto akauliza “Una uhakika gani baba.”

Baba akiwa anarudisha kichwa chake kutoka uelekeo wa dirisha akamjibu “Nafahamu mwanangu.”
.
Yule mtoto alikaa hospitali pale kwa msaada wa mashine kwa mwaka mmoja na akaruhusiwa kurudi nyumbani akiwa na miaka 15 na kukuta barua kitandani

Barua iliandikwa; “ Mwanangu mpendwa kama unasoma barua hii inamaana kila kitu kilienda vizuri kama nilivyokuambia kuwa utapona, siku uliponiuliza nitakupa zawadi gani ya siku yako ya kuzaliwa sikujua ni zawadi gani ningekupa wewe, lakini kwa hali ya sasa ilinibidi nikupe moyo wangu na nakutakia Maisha mema.”

Baba Yule alitoa moyo wake ili binti apone♥

Funzo:

Wapende wazazi wako… wanajitolea sana kutufanya tuwe na furaha bila sisi kufahamu…. Mara nyingi tuko busy tunfanya mambo yetu ya Maisha na kuwasahau wao wakiwa wanazeeka bila ya msaada wetu……Tumia muda wako kuwa na wazazi wako na kuwafanya wenye furaha na upendo wa dhati.

[Kama huwa unawakumbuka wazazi share na comment neno    NAWAPENDA WAZAZI WANGU...]
 

No comments:

Post a Comment