Saturday, 21 December 2013

Shujaa wa muziki wa dansi nchini Muhidin Maalimu Gurumo

CHA KALE DHAHABU


SHUJAA WA MZIKI..TZ
Shujaa wa muziki wa dansi nchini Muhidin Maalimu Gurumo ameliaga
rasmi jukwaa la muziki huo kwa kufanyiwa tamasha maalumu la kumuaga, baada ya kudumu kwa takriban miaka 53 akiimba.
Tamasha hilo lilifanyika Ukumbi wa TTC uliopo Chang’ombe wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam, ambapo pamoja na kujitokeza matatizo ya kiufundi yaliyosababisha kuchelewa kuanza kwake, tamasha hilo lilikuwa na kila aina ya mambo ya kuvutia na kuwaridhisha mashabiki waliofurika kwenye viwanja hivyo.
Pazia la kuagana lafunguliwa
Saa nne usiku, Bendi ya Talent inayoongozwa na mwanamuziki mkongwe, Hussein Jumbe ilifungua jukwaa kwa kuimba wimbo wake wa ‘Pombe nimeikosea heshima’, ulioamsha shangwe za mashabiki waliopamba ukumbi huo.
Wasifu wa Gurumo wawanyamazisha mashabiki
Katika tukio lilivuta zaidi hisia za mashabiki waliotulia kimya wakisikiliza ni wasifu wa mwanamuziki Gurumo uliosomwa na mchambuzi wa muziki Rajabu Zomboko, ambaye pamoja na mambo mengine alieleza maisha ya muziki ya nguli huyo bila kuacha jambo lolote.
Zomboko aliwaduwaza mashabiki alipoeleza kwamba tangu alipoanza muziki rasmi mwaka 1963, Gurumo hajawahi kupumzika kupanda jukwaani, mbali na kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo bendi nyingi huwa mapumzikoni.
Gurumo atangaza warithi wa kazi zake
Katika hali ya kawaida ni jambo gumu kukubali kazi za wengine na kujilinganisha nao hata katika muziki, lakini kwa Gurumo hilo halikuwa hivyo, bali alimtaja Hussein Jumbe kuwa ndiye chaguo lake la kwanza kwa wanamuziki wanaoweza kurithi mikoba yake.
Gurumo alifanya hivyo huku akieleza kuwa anaamini Jumbe anaweza kuyafanya aliyoyafanya yeye akiwa jukwaani ambapo alisema: “Huyu ni chaguo langu la kwanza, atarithi mikoba yangu. Ninamkabidhi maiki hii kama ishara ya kukubali anachokifanya na nina imani atadumu kwenye muziki kama mimi.”
Mkongwe huyo alitoa maneno hayo kisha kumkabidhi kipaza sauti Jumbe, ambaye aliimba wimbo wa Gama uliotungwa na Cosmas Chidumule alipokuwa na Bendi ya DDC Mlimani Park enzi hizo huku akimtaja mwanamuziki Edo Sanga kuwa ni chaguo lake la pili na chaguo lake la tatu lilikuwa ni Juma Katundu.
Alisema kuwa hataki muziki wa dansi ufe, bali uendelezwe na kwamba ndiyo sababu ya yeye kuwachagua wanamuziki vijana na wenye bidii ili wafanye kazi kama aliyofanya yeye kabla ya kuamua kustaafu.
BONYEZA HAPA....UJIPATIE HABARI.
1 | 2

SIMBA DUME

No comments:

Post a Comment