Kijijini
Kijijini nakupenda, kunamahindi nandizi,
Kunayo mengi matunda, kunde, dengu na mbaazi,

Kuna mtamu mlenda, namkumbuka Shangazi,

Mwenzenu ninakupneda, sana kijijini kwetu.


Jamani babu nabibi, kijijini wamepozi,

Jamani kuku wa bibi, na wale wa babu mbuzi,

Nataka kwenda kwa bibi, kula mihogo na ndizi,

Mwenzunu na kukumbuka, sana kijijini kwetu.


Ifikapo asubuhi, JOGO la babangu huwika,

Watu shambani huwahi,ili jembe kulishika,

Ndege nao hufurahi, mitini hufurahika,

Mwenzunu na kukumbuka, sana kijijini kwetu.


Amewaumba billahi, wazuri waloumbika,

Na angani hufurahi, wavutia kwa hakika,

Na Maji nayo Wallahi, TUNGINI yazizimika,

Mwenzetu nakukumbuika, sana kijijini kwetu.