Jamaa mmoja, pengine ni kutokana na imani kubwa kwa serikali hii au ugumu wa maisha, aliamua kudai risiti kwa huduma ya choo baada ya kulipa Tsh. 200. Sakata hili lilitokea karibu na stedi kuu ya mabasi jijini Arusha. Mazungumzo yalianza namna hii:

Mhudumu: Unatakiwa kulipia huduma hii.
Mteja: Shilingi ngapi?
Mhudumu: Mia mbli.
Mteja: Chukua, lakini naomba risiti.
Mhudumu: Risiti ya nini?
Mteja: Ya malipo halali ya Tsh. 200 kama tulivyoagizwa na serikali kudai risiti ili kuchangia pato la taifa!
Mhudumu: Hatujapewa risiti bado na serikali. Hapa watu wote wanatumia huduma bila kudai risiti!

Niliondoka eneo la tukio, sijui nini kiliendelea!!!!