WALIOTOKELEZEA.
Mwanaharakati Maarufu wa Haki za Wamarekani Weusi bwana Malcom x akiwa na Mwanaharakati, Mwanazuoni na Mwanasiasa Nguli wa Tanzania Profesa Abdulrahaman Mohammed Babu miaka ile ya 60.
Babu na Malcom x walikuwa Marafiki sana na Malcom alikuwa Mwanafunzi wa Babu katika mambo mengi ya kiuanaharakati. Unajua walikutana lini?.
LIKE ukurasa "Watanzania Mashuhuri" upate kujifunza zaidi.

Pichani ni Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa Pamoja na Mwigizaji Maarufu wa Marekani Bwana Forest Whitaker ambaye husemwa kuwa Wamefanana sana.
Picha hii ilipigwa wakati Rais Mkapa akiwa katika Awamu ya Pili ya Uongozi wake kati ya Mwaka 2000 na 2005.
Kwa Picha zaidi juu ya waliotokelezea LIKE Ukurasa "Watanzania Mashuhuri" ili ujifunze zaidi.
Picha ni kwa hisani Kubwa ya Mdau wa Ukurasa aliyeko Mafinga huko Iringa.

MUUNGWANA NI VITENDO.
Pichani ni aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwa anazungumza na Mfalme wa Muziki wa Pop Duniani na Mwanamuziki Mashuhuri wa Marekani, Marehemu Michael Joseph Jackson Ikulu Jijini Dar es salaam.
Picha hii ilipigwa Mwaka 1992 wakati Mfalme huyu wa muziki wa Pop wa Marekani, hayati Michael Jackson alipoitembelea Tanzania na kufanya Kitendo cha Kiungwana kwa kufika katika Shule Maalum ya Watoto Yatima na wenye Mtindio wa Ubongo iliyopo Sinza, Jijini Dar es salaam.
Mwanamuziki huyo aliyekuwa maarufu zaidi duniani hadi anakufa 2009, alifika nchini akiwa Balozi wa ziara ya Umoja wa Mataifa na akapokelewa kiserikali na Waziri wa Mambo ya Nje wakati huo, hayati Balozi Ahmed Hassan Diria.
Michael Jackson alitua jioni moja Uwanja wa Ndege wa Dar akiwa amevalia shati la kijani lenye mikono mirefu, suruali nyeusi na kofia nyeusi, akapandishwa kwenye Gari Maalum iliyompeleka hadi Kilimanjaro Hotel (wakati huo) ambayo baadaye ikawa Kilimanjaro Hotel Kempinsk, na sasa ikiitwa Hyatt Regency Dar es Salaam.
Mashabiki waliokuwa na habari walijazana uwanja wa ndege Dar “kumkodolea mimacho” mwanamuziki huyo wakati huo akiwa na umri mdogo tu wa miaka 34, mbali na wale waliomfuata hadi kwenye hoteli hiyo. Wakaungana na wale waliokuwa wakimsubiri hapo kumshangilia kwa mbinja na mayowe ya furaha.
Pia, mashabiki waliokuwa na habari za ujio na ratiba yake, walijitokeza kwa wingi na kumshangaa vilivyo, The Wacko Jacko alipotembelea shule hiyo ya Sinza, kesho yake.
Katika ziara yake hiyo ya siku mbili nchini, alikutana na mkuu wa nchi ambaye wakati huo alikuwa Rais Ali Hassan Mwinyi.
Hivyo Ndivyo Michael Joseph Jackson alivyofika Tanzania na kushikana mikono na watoto wa Sinza miaka karibu 20 iliyopita!.
Picha hii ni sehemu ya Kampeni Maalum ya Ukurasa wa "Watanzania Mashuhuri" ya Kuwafariji na kuhamasisha Msaada na Fursa kwa Watoto Yatima na wale wenye Mtindio wa Ubongo hapa Nchini, Shime Watanzania kila mmoja kwa Nafasi yake tushikamane kwenye hili. Uungwana ni Vitendo.
Picha ni kwa Hisani kubwa ya Idara ya Habari Maelezo.

"IKULU NI MAHALI PATAKATIFU",
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Moja ya nukuu muhimu za Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kuhusu Ikulu, ni pale aliposema “Ikulu ni mahali patakatifu”. Yeye alikaa Ikulu miaka zaidi ya 23 na mpaka anaondoka alikuwa na jeuri na ujasiri wa kusema hadharani kuwa Ikulu ni mahali patakatifu. Watanzania walimwelewa na kumwamini hata kama wanaweza kutofautiana juu ya ni nini hasa kiini cha utakatifu wa Ikulu.
Utakatifu wa Ikulu kwa Baba wa Taifa ulianza mapema kabla hata hajazoea kukaa katika jengo hilo. Kwake yeye, aliona Ikulu ni eneo muhimu kwa utambulisho na utakatifu wa maamuzi ya kila siku kwa taifa. Kutokana na chuki ya Baba wa Taifa kwa ukoloni na wakoloni, alifikia hata kukejeli jumba hilo kwa kuwa lilikaliwa na wakoloni.
Kwa ufahamu na heshima yake kwa kitu kinachoitwa Ikulu, alipata shida sana kuona mtu anawezaje kuishi ikulu kisha akakandamiza, akahujumu uchumi, akaiba, akadanganya, akatukana, akafanya usanii, akafanya uhuni, akadhulumu, akapotosha, akaringia wananchi, akafanya biashara, akapigana na mkewe, au hata kupageuza Ikulu kuwa eneo la kufugia, kutunza ukoo wake na mambo mengine binafsi. Kwake Baba wa Taifa, Ikulu yalikuwa ni madhabahu ya taifa letu, mahali pa kuheshimiwa na kuogopwa.
Haikushangaza wengi, miaka michache baada ya uhuru, Baba wa Taifa alianza jitihada za kuhama Ikulu na kuishi katika nyumba yake binafsi iliyo Msasani. Alifanya hivyo si kwa sababu aliidharau Ikulu ya Magogoni, bali alikuwa anajilinda ili asiingie katika majaribu ya kuigeuza Ikulu kuwa ni nyumba ya ukoo wa Burito.
Aliona Ikulu ni ofisi na alikwenda kazini kama Watanzania wengine, kisha alirudi kulala Msasani katika nyumba aliyojenga mwenyewe kwa mkopo ambao alishindwa hata kuulipa na kukaribia kunyang’anywa.
Kutokana na hofu iliyoambatana na heshima kwa Ikulu yetu, Baba wa Taifa aliona Ikulu pawe ni mahali pa kukaribisha wageni wa kitaifa, kufanya shughuli za ofisi na kufanyia maamuzi muhimu ya kitaifa. Alijua yeye kama mwanadamu anaweza kuwa na hulka zisizohitajika na kuingilia maslahi ya taifa letu.
Hakuwa na maana kuwa marais watakaofuata wasiishi Ikulu kama yeye, bali alilenga kuonyesha eneo lile liwe zaidi ya pango la kuishi wanadamu wenye kutanguliza maslahi yao, familia zao na marafiki zao. Haishangazi kuona leo watu wanahasimiana kutaka kwenda kuishi katika jengo hilo la kikoloni.
Pichani ni Rais wa Kwanza wa Tanganyika na Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa Katika Ofisi yake Ikulu Jijini Dar es salaam.
Picha hii ilipigwa Mwaka 1962. Picha ni kwa Hisani Kubwa ya Hifadha ya Mambo ya Kale ya Serikali ya Uingereza.
Kwa Picha na Maelezo zaidi juu ya Mwalimu Nyerere na Uongozi wake LIKE Ukurasa wa Watanzania Mashuhuri ili upate Kujifunza zaidi.

MTANASHATI WA ZAMANI.
Pichani ni Bwana Ali Sharifu Mussa akionekana Mtanashati sana katika Vazi lake la Asili la Kishirazi.
Ali Sharifu Mussa ambaye alijulikana pia kwa jina la "Baba wa Uvumilivu" alikuwa ni Mmmoja wa Waanzilishi Wakuu wa Chama cha Afroshiraz (ASP) akiwa na kaka yake Othman Sharifu Mussa.
Baadaye Ali Sharifu, Mohammad Hamad Shamte Al-shirazy pamoja na viongozi wenzao wa ASP wa Pemba walijitoa katika Chama cha ASP na kwenda kuasisi chama kipya cha Zanzibar & Pemba People's Party (ZPPP), Unajua kwanini walijitoa?.
Mwanzoni mwa miaaka ya 70 Mzee Ali Sharifu Mussa alipofuka macho kwaajili ya kumlilia nduguye aliyepotea, unamjua huyo nduguye?, unajua kwanini alipotea?.
Kwa yote haya na mengineyo juu ya Watanashati wengine wa zamani Like Ukurasa "Watanzania Mashuhuri" ili upate kujifunza zaidi.
Picha ni kwa hisani kubwa ya Mtoto wa mwisho wa Mzee Ali Sharifu Mussa.
Pichani ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete akionekana Mtanashati katika Shati lake la Gossage, Picha hii inasemekana ilipigwa mwishoni mwa Miaka ya 60 au mwanzoni mwa miaka ya 70.
Shati hili ni sehemu ya Uzalishaji wa Kiwanda Maarufu cha Nguo kilichokuwa Jijini Tanga pale Kwaminchi kilichokuwa kikitengeneza mashati ya lebo maarufu duniani kama vile Gossage, Robin Hood, Arrow, Shikibo na nyinginezo.
Kiwanda kile cha Tanga sasa kimetoweka kwa namna ile ile vilivyotoweka viwanda vingine nchini mwetu.
Unataka kuwajua Watanashati wengine?, Like Ukurasa "Watanzania Mashuhuri" ili upate kujifunza zaidi.
Picha ni kwa hisani kubwa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu.
Pichani ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete akionekana Mtanashati katika Sare zake za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Picha hii inatajwa kupigwa Mwanzoni mwa Miaka ya 80 wakati huo Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Jeshini.
Kwa maelezo zaidi juu ya Maisha ya Mtanashati Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Watanashati wengine wa Zamani LIKE Ukurasa "Watanzania Mashuhuri" upate kujifunza zaidi.
Picha ni kwa hisani kubwa ya Mdau wa Ukurasa aliyeko Mkuranga.
No comments:
Post a Comment