RMTANASHATI WA ZAMANI.
Pichani ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha TANU, Waziri katika Serikali ya Tanganyika, Waziri katika Serikali ya Tanzania, Mwanademokrasia na Mzalendo wa Kweli wa Taifa hili Ndugu Oscar Salathiel Kambona akionekana Mtanashati na Mwenye kupendeza katika Vazi lake la Suti.
Wakati wake Kambona pamoja na kupendwa na Wananchi wote lakini zaidi alipendwa na Wamama kwa sababu ya Utanashati wake na unadhifu wa nywele zake alizopenda kuzichana katika kitindo mbalimbali ambayo watu wengi wa wakati huo walimuiga.
Picha hii ilipigwa Mwanzoni mwa Miaka ya 60 wakati Kambona akiwa na Wazalendo wenzake wakipigania Uhuru.
Kwa maelezo zaidi juu ya Maisha ya Mtanashati Oscar Salathiel Kambona pamoja na Watanashati wengine wa Zamani LIKE Ukurasa "Watanzania Mashuhuri" upate kujifunza zaidi.
Picha ni kwa hisani kubwa ya Mdau wa Ukurasa aliyeko Mbeya.

MUUNGWANA NI VITENDO.
Pichani ni Mwalimu, Mwanaharakati wa Elimu kwa wote, Mjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria na Mzalendo aliyejitoa Mno kwa Watanzania Bibi Barbro Johansson ambaye hujulikana zaidi kwa Jina la "Mama Barbro" (wa Pili kushoto) akiwa pamoja na Aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Tanganyika, Ndugu Julius Kambarage Nyerere (wa kwanza kushoto) pamoja na watu wengine wawili ambao Ukurasa wa "Watanzania Mashuhuri" umeshindwa kuwatambua.
Picha hii ilipigwa Mwaka 1961 Nyumbani kwa Mama Barbro huko Kahororo Bukoba, Mkoani Kagera ikiwa ni Miezi kadhaa kabla ya Uhuru wa Tanganyika.
Mama Barbro aliwasili Nchini Mwaka 1946 kama Mmisheni wa Sweden ambapo anakumbukwa sana kwa Kitendo chake cha Kiungwana cha Kuanzisha Shule ya Kwanza ya Upili ya Wanawake hapa Nchini huko Eneo la Kashasha katika Wilaya ya Bukoba, Mkoani Kagera.
Mwaka 1965 Mama Barbro alijitolea kuiokoa Shule ya Tabora Girls isifungwe kwa kujitolea kuwa Mkuu wa Shule na ndiye Mtu ambaye anasifika sana kwa kuweka Msingi wa Nidhamu katika Shule hiyo.
Mama Barbro hakuishia hapo tu, lakini ndiye Mtu ambaye aliweka Msukumo Mkubwa Mno katika Uanzishwaji wa Sera ya Elimu kwa Watu Wazima hapa Nchini na ndiye mtu ambaye alifanya jitihada za kutosha katika Kampeni ya kuhakikisha Watanzania wanajua kusoma ambapo Tanzania tulifanikiwa na tulipata Tuzo Mbili za Kimataifa za Shirika la UNESCO kwa kutambua Juhudi zetu hizo za kupunguza Ujinga kwa Wananchi.
Mama Barbro alistaafu kuutumika Umma mwaka 1985 na akarudi katika Makazi yake huko Bukoba kabla ya baadaye kuhamishiwa Sweden kwa sababu ya maradhi.
Jijini Dar es ipo Shule ambayo imepewa jina la Barbro Johansson kwa heshima ya Mchango wake kwa Taifa hili, Mfuko wa Ujenzi wa Shule hiyo ulizinduliwa Septemba 25, 1998 Sheraton Hotel, Jijini Dar es salaam na Rais Benjamin William Mkapa ambapo Mama Barbro alihudhuria.
Mama Barbro amefariki Dunia Tarehe 2 Desemba Mwaka 1999 Huko Sweden.
Picha na Maelezo haya ni Sehemu ya Kampeni ya Ukurasa wa "Watanzania Mashuhuri" ya kuwahimiza Watanzania Kuchangia Mfuko wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA) kwa Ajili ya Ujenzi wa Mabweni 30 ya Wasichana Katika Mikoa 8 Tanzania. Kuchangia andika ujumbe CHANGIA TOFALI kwenda namba 15564 (Kila Ujumbe ni Shilingi 250).
Shime Watanzania, Tuchangie. Uungwana ni Vitendo.
Picha na Habari ni kwa Hisani kubwa ya Dada Diana Kamara wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

MTANASHATI WA ZAMANI.
Pichani ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Anne Simamba Makinda akionekana Mtanashati katika Kivazi chake na Namna alivyotengeneza nywele zake.
Picha hii ilipigwa Mwaka 1994 wakati Mama Anne Semamba Makinda akiwa ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto.
Kwa maelezo zaidi juu ya Maisha ya Mtanashati Anne Simamba Makinda pamoja na Watanashati wengine wa Zamani LIKE Ukurasa "Watanzania Mashuhuri" upate kujifunza zaidi.
Picha ni kwa hisani kubwa ya Mdau wa Ukurasa aliyeko Iringa.

WALOTOKELEZEA.
Pichani ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Bwana Freeman Aikaeli Mbowe (wa Pili kutoka Kushoto) akiwa Pamoja na Mwanamuziki Nguli kutoka Zaire (Sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo) Bwana Koffi Antoine Olomide (wa Tatu kutoka Kushoto waliokaa).
Bwana Freeman Aikaeli Mbowe na wenzie waliopo kwenye Picha ndio waliofanikisha Ziara ya Kwanza ya Mwanamuziki huyo Mashuhuri wa Afrika Nchini katika Miaka ya 90 Mwanzoni, Wa Kwanza kulia waliokaa ni Bwana Ronie Mtawali ambaye alikuwa Meneja wa Kwanza wa Club Billicanas.
Kwa Picha zaidi juu ya waliotokelezea LIKE Ukurasa "Watanzania Mashuhuri" ili ujifunze zaidi.
Picha ni kwa hisani Kubwa ya Blogu ya "Michuzi" ya Mpiga Picha Mashuhuri Tanzania, Bwana Muhidini Issa Michuzi.

- HAPPY BIRTHDAY MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD.
Maalim Seif Shariff Hamad ni Katibu Mkuu wa chama cha upinzani CUF (Chama cha Wananchi) na Pia Makamo wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Alizaliwa 22 Oktoba mwaka 1943, katika kijiji cha Nyali, Mtambwe kisiwani Pemba, Tanzania.
Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Uondwe, 1950 na baadaye alijiunga na elimu ya sekondari katika shule ya wavulana Wete Pemba 1952. Baadaye aliendelea na elimu ya sekondari katika shule ya King George VI (Sasa Lumumba College) na kuhitimu kidato cha sita mwaka 1963, Shuleni hapo Mmmoja wa Walimu wake akiwa ni Rais Aboud Jumbe Mwinyi.
Mara baada Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 Mzee Karume hakutoa nafasi kwa Wanafunzi Kujiunga na Fursa za kujiendeleza kwa Elimu ya Juu zaidi ya Ualimu hivyo ilimbidi Maalim Seif naye ajikite katika Ualimu wa Skuli Mbalimbali huko Zanzibar.
Mwaka 1972 Mara baada ya Kifo cha Rais Amani Abedi Karume na Mzee Aboud Jumbe kuchukua Uongozi ndipo milango ya fursa za kujiendeleza kwa elimu ya Juu kwa Vijana wa Kizanzibari ilipofunguliwa, Vijana Maalim Seif Shariff Hamad, Juma Duni Haji, Ramadhaan Omari Mapuri na wenziwao wakawa Vijana wa Kwanza wa Kinzanzibari kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Historia ya Maalim kwenye Siasa za Tanzania ni ndefu, leo katika hii siku muhimu kwake utoshe utambulisho huo mchache.
Pichani ni Maalim Seif Shariff Hamad akiwa na Viongozi wenzake wa Serikali, Picha hii ilipigwa Mwaka 1985 wakati Maalim akiwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ukurasa wa "Watanzania Mashuhuri" unamtakia Maalim Seif Shariff Hamad Furaha ya Siku ya Kuzaliwa na unampongeza kwa kutimiza Umri wa Miaka 69 katika Maisha yake. Mola ampe Afya Njema na ampe uwezo katika na Utekelezaji wa Majukumu yake ya kuutumikia Umma.
Happy Birthday Maalim Seif Shariff Hamad. - FAHARI YETU.
Pichani ni Wanamuziki wa Kundi Mashuhuri la Taarab lijulikanalo kama Nadi Ikhwani Safaa la Malindi huko Zanzibar wakitoa Burudani ya kuvutia kwa Washabiki wao katika Moja ya Maonyesho yao mbalimbali.
Kundi hili la Taarab lili...See more - WALIOTOKELEZEA.
Pichani ni Aliyekuwa Waziri wa Elimu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Katibu wa Mipango na Uchumi wa Chama cha Mapinduzi CCM, Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Kiongozi wa Kundi la Wataka Mabadiliko Za...See more - MTANASHATI WA ZAMANI.
Pichani ni aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Rais wa ASP, Muasisi wa Muungano wa Tanzania na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheikh Abedi Amani Kar...See more - MUUNGWANA NI VITENDO.
Lugha ya Watu ni Kitu adhimu mno katika Maisha yao, lakini pia i Utambulisho wao Mkuu na pia ni nembo ya Taifa lao popote walipo Duniani. Kiswahili inatajwa kama Lugha Rasmi ya Taifa ya Tanzania japo Matumizi yake kwe...See more - FAHARI YETU.
Utaifa ni Jambo zito na la Fahari sana kwetu, Ni Utambulisho wetu kama wanataifa popote tulipo Duniani na ni kielelezo cha Utu na Asili yetu kama Wanaadamu.
Mavazi ni nembo Muhimu sana katika kudumisha mila za Utaifa wetu na ...See more - MUUNGWANA NI VITENDO.
Kama Taifa tumetoka mbali sana na tumevumiliana katika Mengi, Wazee wetu pamoja na Tofauti zao za Kikabila, Kiitikadi, Kidini na Kiuchumi waliishi vyema na kwa Amani katika Misingi ya Utu, Upendo wa hali ya Juu, kuhes...See more - WALIOTOKELEZEA.
Pichani ni Aliyekuwa Katibu wa Mipango na Uenezi wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha TANU, Mmoja wa Wabunge wa Mwanzoni Wanawake wa Bunge la Tanganyika na kisha Tanzania, Mtetezi wa Harakati za Ukombozi wa Wanawake, Mpigania ...See more - MTANASHATI WA ZAMANI.
Pichani ni Mpigania Uhuru, Mwanaharakati wa Haki za Wanawake, Mwandishi Mahiri wa Vitabu na Mzalendo Mashuhuri wa Tanzania Bibi Sophia Mustafa akionekana Mtanashati sana Katika Vazi lake la "Sari".
Picha hii ilipigwa...See more - MUUNGWANA NI VITENDO.
"Mimi nimeamua kujitoa mhanga kwa ajili ya kuwaokoa vijana wenzangu. Siogopi hata kufa kwa kusema ukweli".
Maneno haya Mazito yenye kuonyesha Dhamira ya Kweli, Nia Thabiti na Uwezo usio na shaka wa Kupambana Dhidi y...See more - WALIOTOKELEZEA.
Pichani ni Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa Pamoja na Mwigizaji Maarufu wa Marekani Bwana Forest Whitaker ambaye husemwa kuwa Wamefanana sana.
Picha hii ilipigwa wakati Rais Mkapa akiwa katika...See more - MTANASHATI WA ZAMANI.
Pichani ni Mwanaharakati Nguli wa Uhuru, Mtaalam Hodari wa Kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Makerere na Mmmoja wa Wazalendo wa Kupigiwa Mfano wa Taifa hili Mtemi Abdallah Said Fundikira III, Chifu wa Unyanyembe, akionekan...See more - MUUNGWANA NI VITENDO.
Anaitwa Mbaraka Mwinshehe Mwaruka japo Vijana wenzie wa Zamani walipenda kumuita majina Mbalimbali kulingana na Umahiri wake katika Kutunga, kuimba na Kupiga Gitaa akiwa katika Bendi ya Morogoro Jazz mpaka alipounda B...See more - WALIOTOKELEZEA.
Pichani Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Makamo wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Chama cha ASP akiwa pamoja na Baadhi ya Wanamapinduzi ambao walishiriki Katika ...See more - MTANASHATI WA ZAMANI.
Pichani ni Mwanazuoni Nguli, Mchumi Mwenye Uwezo na Msomi Maarufu wa Kitanzania Profesa Justian Ferdinand Rweyemamu ambaye anaonekana Mtanashati Katika Vazi lake la Suti.
Picha hii ilipigwa Mwaka 1965 wakati Profesa...See more - BAYUME MOHAMED HUSSEIN, MTANZANIA MASHUHURI ALIYEUAWA NA HITLER.
ALIVYOTAJIKA.
Je, ni jina jipya?, Geni au umewahi kulisikia sehemu?. Hebu leo jipe muda kumuangalia Mtanzania huyu wa tangu na Mmashuhuri wa leo katika Ukurasa huu wa "Wata...See more
No comments:
Post a Comment