*******
SAMAMDOE:
Huyu ndo chizi kweli
James ni mfungwa katika gereza la machizi,siku moja akawaambia marafiki zake,''naanza kufanya mazoezi ya kuruka geti ili baada ya miezi mitano nitoroke kwa kuruka geti'' james akaanza mazoezi ya kuruka,muda ulipofika akawaaga machizi wenzie akawaambia ''leo nakwenda kuruka geti nitoroke'' akaondoka,baada ya muda kidogo james akarudi huku amenyong'onyea,wenzake wakamuuliza,mbona umerudi?james akajibu ''nimeshindwa kuruka geti na kutoroka kwa sababu geti lilikuwa wazi''******
SAMACHAU:
Yesu na Wanafunzi wake
Siku moja Yesu alikuwa na wanafunzi wake nyikani, baada ya mafundisho marefu na jua kali wanafunzi wake walihisi njaa. Yesu alifahamu mawazo yao akasema,"Petro kalete jiwe", Petro alinyanyuka na baada ya muda alirudi akiwa na jiwe mkononi. Alipompa Yesu akalibariki likawa mkate, akawagawia wanafunzi wake wakala. Lakini hawakushiba hivyo wakaanza kumlaumu Petro,.."mbona umeleta jiwe dogo?", Petro akawajibu,"me nilijua mwalimu anataka kukalia!".Siku nyingine tena wakiwa nyikani, baada ya mafundisho marefu na jua kali, wanafunzi walihisi njaa. Yesu alifahamu mawazo yao, akasema "Petro kalete jiwe". Basi walinyanyuka wanafunzi kama 6 hivi, wakaleta jiwe kubwa huku wakilibiringisha. Walipolifikisha Yesu alilikalia na kuanza kuwafundisha neno!!
hahahahahahahahaaaaahhahaha!!!
No comments:
Post a Comment