usiku wa bikidude, usiku wa wanawake
ziff, jukwaa la wanawake
WANAMUZIKI Nguli nchini wakiongozwa na Sit Bin Saad ambaye ni mjukuu wa marehemu Bi.Kidude,Synerg, Baby J wote hawa ni kutoka Zanzibar Linah na THT Band kutoka Dar es Salaam kesho watawasha moto ndani ya mabo klabu kwa ajili ya kumuenzi marehemu Bi.Kidude ambaye aliwahi kutumbuiza katika matamasha ya ZIFF yaliyowahi kufanyika.
Tamasha la filamu la nchi za Jahazi maarufu kama ZIFF linaendelea
kupamba moto na kesho ni usiku maalumu wa wanawake katika kumuenzi
marehemu Bi.Kidude katika tamasha hilo.
Tamasha hilo ambalo lina siku ya 5 tangu kuanza kwake limekuwa ni
kivutio kikubwa kwa wakazi na wageni kutoka kila kona ya dunia
kuwapa burudani kulingana na mahitaji.
Usiku wa wanawake utafanyika leo(kesho) ndani ya mambo
klabu ampapo wasanii watakao tumbuiza katika tamasha hio watakuwa ni
wanawake pekee ambapo mjukuu wa marehemu Bi.KIdude atafungua
dimba kutoa burudani hiyo.
Wanawake wameombwa kuhudhuria kwa wingi kwakuwa tamasha la siku
ya leo ni kwa ajili ya wanawake.
katika tamasha hilo la usiku wa wanawake wasanii hao wataweza kukonga
nyoyo za mashabiki wake na kufanya kufana kwa tamasha hilo ambalo linamkumbuka
Bi.kidude kwa mchango wake ambao alikuwa akiutoa katika kipindi chake
chote cha uhai wake.
No comments:
Post a Comment