Vijana wengi ambao wanapendana leo
Vijana wengi ambao wanapendana leo
Vijana wengi ambao wanapendana leo
mapenzi yao hayadumu kiasi cha
kubatishwa jina la utamu wa bazoka.
Lakini yote hii inatokana na ukweli
kwamba elimu ya mapenzi ambayo ni
muhimu kwa binadamu haitolewi ipasavyo.
Ipo zana potofu kwamba kumfundisha
motto mapenzi ni kumharibu, jambo
ambalo si kweli bali inategemea mtoto
huyo anafundishwa nini na kwa wakati
gani. Lakini cha kushangaza zaidi hata watu wazima ambao ni wadau wa
mapenzi hawayajui, matokeo yake
wanajiingiza kwenye uhusiano wakiwa
bumbumbu na hivyo kuteshwa na
changamoto za mepenzi.
Leo tutajifunza kwa undani sifa kumi za mpenzi bora ili tuweze kuwatambua
wapenzi wetu kabla ya kuwapa mioyo na
utu wetu. Sifa hizo hizi zifuatazo.
1. Mpenzi wa kweli ni yule ambaye
hatangoja kujua nini unahitaji yaani hana
sababu ya kusubiri kuombwa ndiyo atoe msaada.
2. Ni yule atakayejua wakati gani huna
furaha au una furaha na atakuwa na
wewe kwa hali zote mbili .
3. Ni yule atayekuwa tayari kukusikiliza
kwa kile utakachosema, hatojali umeongea baya au zuri .
4. Atakuwa na wewe wakati wa shida na
raha. Hatakuacha mtu wa kuvizia vizia na
kujisogeza wakati ukiwa na raha.
5. Mpenzi wa kweli atakuheshimu na
hatopenda kuwa nyuma na kukuacha bila msaada .
6.Atakupenda kwa moyo wake wote na
wala si kwa ajili ya shinikizo fulani (pesa
au mali)
7.Mpenzi wa kweli ni yule
atakayeonyesha kuthamini nafasi yako kama rafiki au mpenzi mbele ya wengine
8. Kwenye ukweli mpenzi mzuri atasema
bila kukuficha na atapenda kukuonyesha
mifano ya namna ya kuwa mkweli na
mwaminifu.
9. Mpenzi wa kweli ni yule anayejiamini, asiyeyumba katika maamuzi hata kama
atalazimika kufanya maamuzi magumu .
10.Atakuwa tayari kuvumilia, hatakuwa
mwepesi wa hasira wala kutumia lugha
chafu na ubabe.
No comments:
Post a Comment