KILIMANJARO
AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA
KUGHUSI SAINI YA PINDA
MFANYABIASHARA Amadi Ally Popi (35), jana alifikishwa mbele ya Hakimu
Mkazi wa MAhakama ya Hakimu Mkazi Kisutu – Dar es Salaam, Waliarwande
Lema akishtakiwa kwa makosa mawili likiwemo la kughushi barua
inayoonyesha imeandikwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Inspekta
wa Polisi Hamis Said, aliiambia Mahakama kuwa tarehe na siku
isiyofahamika ndani ya jiji la Dar es Salaam, kwa nia ya kudanganya
Amadi Ally Popi alighushi barua yenye kumbukumbu Na. DA21/3078/01A/142
ya Desemba 3, 2012 akijaribu kuonyesha kuwa barua hiyo ni halali na
ilikuwa imeandikwa na kusainiwa na Waziri Mkuu, Pinda.
Alidai shtaka lingine ni kuwa tarehe na siku isiyofahamika ndani ya
jiji la Dar es Salaam, bila ya kuwa na mamlaka yoyote alitengeneza barua
hiyo na kuisani na kisha alimpatia Islamu Mohammed Mtila akijaribu
kuonyesha barua hiyo imetoka katika Ofisi ya Waziri Mkuu na imesainiwa
na Pinda.
Mshtakiwa alikana tuhuma hizo na kupelekwa rumande
hadi tarehe 5-Septemba kesi hiyo itapotajwa tena. Hii ilikuwa ni baada
ya mstakiwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini
wawili wanaofanya kazi serikalini au kwenye taasisi zinazofahamika
watakaosaini bondi ya sh milioni 10.
MBUGA ZA WANYAMA.. Tz |
No comments:
Post a Comment