CHUI WA TANZANIA |
Dalili ya anayejirudi
kwa mpenzi wake wa zamani
TUNDA LA UPENDO.. |
NAKUSHURU wewe unayeguswa na safu hii kiasi
cha
kuniunga mkono kila kila Jumamosi katika kujadili mambo yanayohusu mambo ya
uhusiano na maisha katika jamii yetu.
MANSHALAAAA. |
Nitakuwa mchoyo wa fadhira kama nitashindwa kukushuru
na kukutakia kheri pia wewe unayeona umuhimu wa kuipitia safu hii.
Ndugu msomaji wangu, katika uhusiano wa
kimapenzi, kumekuwa na mapungufu mengi yanayoweza kutokea katika jamii yetu.
Hii ni pale mtu anaposhindwa kujizuia na mpenzi
wake wa zamani kiasi cha kutia shaka. Hapo awali nilishawahi kuijadili suala
hili.
Hata hivyo, suala hili ni pana mno. Wengi
linawakabiri na kuwachanganya kisaikolojia. Kuna mengi yanaweza kutokea ndani
yake, ila hii ni dalili ya wazi kuwa mtu wako anaendelea kumpenda aliyeachana
naye.
Kuna watu ambao licha ya kuachana na wapenzi wao
wa zamani, lakini bado hawawezi kuwa mbali nao kwa kiasi kikubwa.
Kwa mfano, kuna mtu ambaye muda mwingi anakesha
katika albamu akimuangalia mpenzi wake huyo aliyeachana naye.
Kama sio albamu, pia ni ngumu kumshauri azitupe
au kuzirejesha nguo zilizokuwa zinatumiwa na mpenzi wake wa zamani ili kuondoa
usumbufu.
Kuna msomaji wangu mmoja ameonyesha kuumizwa
kichwa na suala hili. Huyu alisema kuwa ana mpenzi wake, ila anamshangaa
anapozihifadhi nguo na vitu vyote vilivyokuwa vinatumiwa na mtu wake.
Mbaya zaidi, alipoamua kuzichoma baadhi yake,
aliingia kwenye kadhia ya kutukanwa na mtu huyo. Hili ni jambo la kushangaza
mno.
Wewe kama umeachana na mtu wako, unawezaje
kuhifadhi vitu vinavyoweza kukumbusha matukio ya nyuma?
Kwanini uishi kwa kumsumbua mwenzako hadi
ashindwe kulala usingizi kwa sababu yako binafsi? Ni wazi mtu yoyote mwenye
mtazamo huu, basi ni ishara kuwa hawajaachana.
Hata kama ameachana naye, basi si chache zijazo
atarudiana naye. Wewe uliyekuwa kwenye uhusiano wa aina hiyo lazima uwe makini.
Nasema hivyo kwasababu kama upon a mtu ambaye
muda mwingi anashindwa kumsahau mpenzi wake wa zamani, ni wazi kuwa uwapo una
mashaka.
Huenda ameshindwa kabisa kutulia kutokana na
nafasi yako, hivyo ni wakati wako kuumiza kichwa kwa ajili ya kujua cha
kufanya.
Inawezekana kabisa ukawa kwenye hisia na mpenzi
wako wa zamani, ila kwakuwa umeshaachana naye kwanini ushindwe kumsahau?
Ili tuweze kufurahia mapenzi, lazima tuwe makini
katika mambo yetu. Hakuna haja ya kujiingiza katika uhusiano ambao una mashaka.
Kwa wewe uliyekuwa kwenye uhusiano wa aina hiyo,
unapaswa ujiangalie ili usiingie kwenye wasiwasi wa kujipotezea muda wako.
Hakuna haja ya kuishi kwa wasiwasi kwasababu ya
mtu ambaye anashindwa kabisa kujisahaulisha ili aweze kutumia muda huo kulipa
fadhira ya upendo wako.
Ni wakati wako kujua kuwa kama upo kwenye
uhusiano na mtu ambaye chumbani kwake amehifadhi nguo au vitu vingine vya mtu
wake wa zamani kuwa bado anamuwaza na hawezi kumsahau.
Mbaya zaidi pale unapomshauri mazuri yeye
akakuona huna lolote la kumwambia kwa ajili ya maisha ya upendo wenu kwa
ujumla.
Hayo ni mapenzi yenye kuumiza kichwa. Kama mtu
anashindwa kumsahau mtu wake huyo, basi wakati wowote mapenzi yao yataanza
upya.
Ndio hao licha ya kuachana na mtu, lakini muda
mrefu wapo katika mawasiliano kiasi cha kuibua maswali lukuki kutoka kwenye
jamii.
Huo ndio ukweli wa mambo, hivyo lazima kila
mmoja wetu awe makini kama ana lengo la kujipa furaha katika moyo wake,
vinginevyo ni maumivu.
Tukutane wiki ijayo.
ZUGUA SIMO NA NJERO |
No comments:
Post a Comment