ZIGUA SIMO NA NJERO |
Huenda Handeni CAF ikapoteza wanachama na viongozi kwani ni baada ya mgombea nafasi ya ubunge kapitia chama hicha Mheshimiwa Remmy Aidan Shundi kukumbana na majukumu mengi ya Kitaifa na kusababisha kishindwa kuendelelea na shughuli za Kisiasa hatahivyo huenda ni moja ya mbinu mpya atakazo rudi nazi katika katika awamu yapili hapo mwaka 2015 zitakuwa za kisasa zaidi hata hivyo....
MKURUGENZI wa Siasa na Uenezi wa wilaya Handeni mkoani Tanga wa Chama Cha Wananchi (CUF), Zuberi Mussa Abdulrahman, amesema hana haja ya kukaa kwenye chama kisichojitambua, ndio maana ameamua kurudi kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wafuasi wa CUF wakiwa kwenye mikutano ya chama chao.
Bosi huyo wa zamani wa
CUF wilayani Handeni sasa yupo CCM baada ya kukiacha chama hicho kwa kipindi
cha miezi miwili, huku akisema hakina mashiko na kimepoteza dira.
Akizungumza na Handeni
Kwetu Blog, Mussa alisema CCM imekuwa ikifanya siasa safi na dhamira ya
kuwaongoza Watanzania wote, hivyo kwake yeye kuhama CUF ni jambo la busara mno.
Alisema anaamini kwa
sasa atashirikiana na viongozi wa CCM ili kufanikisha maendeleo ya Handeni na
Tanzania kwa ujumla, chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi.
“Siwezi kukaa kwenye
chama ambacho sera yake haijulikani na kuchelewesha maendeleo ya Taifa kwa
ujumla, ukizingatia kuwa kwa muda mrefu sasa CUF imekosa mashiko.
“Tangu nilipokihama
rasmi miezi miwili iliyopita na kurudi CCM, maisha yangu yamekuwa na furaha kwa
kuona wananchi wanashirikiana kwa kiasi kikubwa na serikali yao inayojali
maisha yao,” alisema.
Kuhama kwa Mussa ni
muendelezo mbaya wa maisha ya chama cha CUF wilayani Handeni mkoani Tanga, huku
idadi kubwa ya viongozi wao wakiwa na lengo laa kukimbia na kuhamia kwenye
vyama vingine vya siasa.
Tanzania Nchi yangu nakupenda |
No comments:
Post a Comment