
KILIMANJARO 

 
 BAADHI ya wabunge wamekosoa mbio za Mwenge wa Uhuru, huku wengine 
wakitaka ufutwe kwa maelezo kuwa hauna tija kwa sasa. Wabunge hao 
wakiwamo wa upinzani na CCM, walisema Mwenge umekuwa kero na kwamba 
wakati mwingine ofisi za umma hufungwa kutokana na mbio zake na hivyo 
kusababisha wananchi kukosa huduma.
 
 Sakata hilo lilitokea jana 
Bungeni mjini Dodoma, baada ya Mbunge wa Musoma Mjini Vicent Nyerere 
(CHADEMA) kutaka kujua faida na hasara zilizopatikana tangu Mwenge wa 
Uhuru ulipoanza kukimbizwa katika maeneo mbalimbali nchini.
 
 

Nyerere alisema wakati fulani viongozi wa Serikali walimtisha Naibu 
Meya wa Manispaa ya Musoma, Nyamero Bwire, kutokana na hatua yake ya 
kuzuia gari la wagonjwa la hospitali ya wilaya kutumika katika mbio 
hizo.
 
 Katika swali lake la msingi, mbunge huyo aliuliza kwamba 
“kwa kuwa tangu mwenge ulipohamishiwa katika mfumo wa Serikali, wananchi
 wamekuwa wakilazimishwa kuchangia fedha kwa nguvu pamoja na matumizi 
yasiyokuwa sahihi ya magari ya Serikali. Je, Serikali haioni kwamba 
kuanzia sasa ianze kukimbiza mwenge katika maeneo yale tu ambayo 
wananchi wake wapo tayari kuchangia michango ya mwenge?” 
 
 
Aidha, Mbunge huyo pia alitaka kujua kiasi cha bajeti ya mbio za mwenge 
kwa mwaka na iwapo matumizi ya fedha hizo hufanyiwa ukaguzi.
 
 
Kwa upande wake Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Kesy (CCM), alisema mbio
 za mwenge hazina faida kwa Watanzania walio wengi kwani shughuli za 
kiuchumi zimekuwa zikiathiriwa.
 
 “Binafsi hiki kitu kinachoitwa 
mwenge sikitaki kabisa, kwani ni wazi tangu maandalizi yake hadi kufika 
kwake kumekuwa na mateso, kwani viongozi wanatakiwa kutoa huduma lakini 
wote huondoka ofisini.
 
 “Wanatumia siku tatu kwa ajili ya 
kukagua miradi inayoitwa ya mwenge, huku wananchi wakisota kuwasubiri na
 hata baada ya kufika na kukesha katika eneo husika.
 
 “Wakati 
mwingine hutumia siku mbili kupumzika badala ya kuwahudumia wananchi kwa
 kisingizio cha mwenge. Sasa tulipofika inatosha, ni vema mwenge 
usikimbizwe kwani umekuwa na matumizi mabaya,” alisema Kesy.
 
 
Baada ya maswali hayo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Utawala Bora, 
George Mkuchika, alisimimama kujibu kwa kwa kusema “Wale wanaodai kwamba
 mbio za mwenge hazina umuhimu si kweli. Malengo yake yalikuwa ni 
kukimbizwa Tanganyika na umekuwa ukitoa elimu kama vile elimu kuhusu 
dawa za kulevya, rushwa na kuzindua miradi ya maendeleo.” 
 
 Hata
 hivyo majibu hayo yalimfanya akumbane na zomea zomea kutoka kwa wabunge
 wa kambi ya upinzani, huku zikisikika sauti za wabunge wakisema; 
“Mwenge unaeneza Ukimwi”, “unaeneza ufisadi na hatuutaki tena”.
|  | 
| KILIMANJARO | 

BAADHI ya wabunge wamekosoa mbio za Mwenge wa Uhuru, huku wengine wakitaka ufutwe kwa maelezo kuwa hauna tija kwa sasa. Wabunge hao wakiwamo wa upinzani na CCM, walisema Mwenge umekuwa kero na kwamba wakati mwingine ofisi za umma hufungwa kutokana na mbio zake na hivyo kusababisha wananchi kukosa huduma.
Sakata hilo lilitokea jana Bungeni mjini Dodoma, baada ya Mbunge wa Musoma Mjini Vicent Nyerere (CHADEMA) kutaka kujua faida na hasara zilizopatikana tangu Mwenge wa Uhuru ulipoanza kukimbizwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Katika swali lake la msingi, mbunge huyo aliuliza kwamba “kwa kuwa tangu mwenge ulipohamishiwa katika mfumo wa Serikali, wananchi wamekuwa wakilazimishwa kuchangia fedha kwa nguvu pamoja na matumizi yasiyokuwa sahihi ya magari ya Serikali. Je, Serikali haioni kwamba kuanzia sasa ianze kukimbiza mwenge katika maeneo yale tu ambayo wananchi wake wapo tayari kuchangia michango ya mwenge?”
Aidha, Mbunge huyo pia alitaka kujua kiasi cha bajeti ya mbio za mwenge kwa mwaka na iwapo matumizi ya fedha hizo hufanyiwa ukaguzi.
Kwa upande wake Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Kesy (CCM), alisema mbio za mwenge hazina faida kwa Watanzania walio wengi kwani shughuli za kiuchumi zimekuwa zikiathiriwa.
“Binafsi hiki kitu kinachoitwa mwenge sikitaki kabisa, kwani ni wazi tangu maandalizi yake hadi kufika kwake kumekuwa na mateso, kwani viongozi wanatakiwa kutoa huduma lakini wote huondoka ofisini.
“Wanatumia siku tatu kwa ajili ya kukagua miradi inayoitwa ya mwenge, huku wananchi wakisota kuwasubiri na hata baada ya kufika na kukesha katika eneo husika.
“Wakati mwingine hutumia siku mbili kupumzika badala ya kuwahudumia wananchi kwa kisingizio cha mwenge. Sasa tulipofika inatosha, ni vema mwenge usikimbizwe kwani umekuwa na matumizi mabaya,” alisema Kesy.
Baada ya maswali hayo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Utawala Bora, George Mkuchika, alisimimama kujibu kwa kwa kusema “Wale wanaodai kwamba mbio za mwenge hazina umuhimu si kweli. Malengo yake yalikuwa ni kukimbizwa Tanganyika na umekuwa ukitoa elimu kama vile elimu kuhusu dawa za kulevya, rushwa na kuzindua miradi ya maendeleo.”
Hata hivyo majibu hayo yalimfanya akumbane na zomea zomea kutoka kwa wabunge wa kambi ya upinzani, huku zikisikika sauti za wabunge wakisema; “Mwenge unaeneza Ukimwi”, “unaeneza ufisadi na hatuutaki tena”.

No comments:
Post a Comment