Saturday, 31 August 2013

WATANZANIA NI MAKULI WA KUBEBA MADAWA YA KULEVYA ....."2"




Zigua Simo na Njero

Mtoto wa Kiafrica
Uchunguzi wetu ulibaini kuwa unaweza kununua kinyago cha kimakonde na kukitoboa katikati kisha kuhifadhi cocaine, heroin au mandrax ndani kisha
kukifunga vyema kama mzigo katika boksi na kuutuma katika nchi unayoitaka.
UGA WA SEMBE
Hata hivyo, mbinu maarufu inayotumiwa na Watanzania wengi ni kumeza pakti za dawa za kulevya na kusafiri kwa njia ya basi hadi Afrika Kusini kisha kuvitoa kwa njia ya haja kubwa baada ya kufika.
Njia hii imekuwa na athari kiasi cha baadhi ya wasafirishaji kupoteza maisha; Mfano ni Watanzania wawili, Hassan Wanyama na Ali Mpili ambao walifariki mwaka jana kwa kumeza dawa hizo kisha kupasukia tumboni.
Mpili alifia katika nyumba ya wageni ya Braeside, Harare baada ya kukosa basi la moja kwa moja kwenda Afrika Kusini hivyo dawa hizo kupasukia tumboni.
Mpili alikuwa amemeza kete zaidi ya 80 za heroin.Watanzania wawili waliokuwa wakifanya mbinu za kuutorosha mwili wa Mpili nao walikamatwa.
UNGA WA DONA
Watanzania kukithiri katika biashara ya dawa za kulevya
kumesababisha wengi hata wale waaminifu kuingia katika usumbufu mkubwa na kubatizwa majina chekwa yanayohusiana na dawa za kulevya.
“Mipakani siku hizi sisi Watanzania tunapekuliwa kivyetu, wakituona tu wanatuita ‘drugs’ tofauti na zamani tulijulikana kama taifa lenye watu watakatifu,” kinasema chanzo hicho.
Msemaji wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini (TDCC) Florence Mlay alizungumza na Mwananchi na kueleza kuwa, tume hiyo bado haina taarifa rasmi kuhusu ongezeko la watumiaji na wafanyabiashara wa dawa za kulevya Afrika Kusini.
BWIMBWI
“Kwa sasa hatuna ripoti yoyote kuhusu Watanzania Afrika Kusini, lakini kwa kuwa vyombo vya habari vinajitahidi kwa kasi basi tutalifanyia kazi hilo,” alisema Mlay.
Mipaka ya Tanzania
Tanzania kutumika kama moja ya njia kuu za kusafirisha mihadarati kunathibitishwa na tukio la Julai 2012 ambapo Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini (SARS) ilikamata kiasi cha kilo 350 cha dawa haramu aina ya Mandrax zikitokea Tanzania, kisha zilipita Botswan na baadaye kuingia Afrika Kusini.
UNGA WA NGANO
Julai mwaka huu, wanawake wawili wa Kitanzania Agnes Masogange na Melissa Edward walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo na mabegi sita yaliyosheheni dawa za kulevya aina ya methamphetamine maarufu kama `Tik’ yenye thamani ya Sh7 bilioni.
1 | 2 | 3 Next Page»
TANZANIA

 
 
 

No comments:

Post a Comment