Mdogo wake marehemu Kanumba aibuka
jijini Dar es Salaam na kutoa maneno mazito, amlillia kaka yake,
apata msoto kulilia sanaa ya Tanzania
MDOGO wake marehemu
Steven Charles Kanumba, anayeitwa Lameck Charles Kanumba, ameibukia jijini Dar
es Salaam, huku akisema kuwa kaka yake anamtokea ndotoni na kuzungumza naye
mambo mengi, yanayohusu familia na sanaa ya Tanzania.
Lameck Charles Kanumba anavyoonekana kwa karibu, baada ya kuzungumza mengi na Handeni Kwetu Blog.
Lameck aliyasema hayo
mapema leo mchana, ikiwa ni miezi mine tangu alipokuja jijini Dar es Salaam
kwenye kumbukumbu ya kaka yake, ambapo pia historia inafanana kutokana na baba
yao kuendelea kula kona na kuacha kuwatunza watoto wake na kuwatelekeza kwa
mama zao.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa, Lameck alisema kuwa kwa sasa yupo jijini Dar es Salaam, ambapo pia anatumia nafasi hiyo kuhangaikia masuala ya sanaa ambayo yapo kwenye damu yake.
Alisema hawajawahi kuonana uso uso kwa Kanumba, kutokana na yeye kuishi mkoani Mbeya na mama yake, wakati siku anakufa alishindwa kupata nauli ya kuja kwenye mazishi yake.
“Naendelea kuumia
kutokana na kufariki kwa kaka kabla ya kuzungumza naye uso kwa uso, lakini pia
inashangaza kwakuwa mara kadhaa huwa ananijia ndotoni na kuzungumza naye hasa
mambo yanayohusu familia.
“Baba hajanihudumia
tangu mtoto kama ilivyokuwa kwa kaka Kanumba, hivyo bado naona nina mengi ya
kufanya kwa ajili ya kumuenzi marehemu aliyeifanyia mambo mema Tanzania kwa
kupitia sanaa,” alisema.
Aidha, Lameck yupo
katika maandalizi kabambe ya kuandaa filamu yake inayojulikana kwa jina la ‘Charles’,
huku akiishi kwa msamaria mwema, anayelikana kwa jina la Fatuma au mama Kenge,
mtaa wa Sinza Uzuri, jijini Dar es Salaam.
TEMBO |
No comments:
Post a Comment