|
Tembo wa Tanzania |
|
|
|
|
| |
Jicho la Africa |
|
Mapambano D.R.Congo |
|
Wanajeshi -DRC |
Vikosi vya serikali ya Congo na wapiganaji waasi wamepambana
Daktari mmoja aliyekuwa mstari wa mbele katika mapigano hayo amesema
huduma za afya zimepata changamoto kubwa kutokana na majeruhi wengi.
Mapigano baina ya jeshi la serikali na kundi la waasi wa M23 yalidumu
usiku kucha kuanzia Jumamosi hadi Jumapili huko Mujoga takriban kilomita
17 kaskazini mwa Goma.
Daktari Isaac Warwanamiza ameiambia Sauti ya Amerika kwa njia ya simu
alikuwa hospitali pamoja na Watanzania walioko katika jeshi la Umoja wa
Mataifa wakisubiri kwenda mstari wa mbele na kwamba wote waliomzunguuka
waliuawa na wengine wengi ni majeruhi.Alisema kufikia Jumapili asubuhi
watu 82 walikuwa wameuawa.
Wakati, huo, huo Marekani imesema imeshtushwa na ghasia zinazoendelea
baina ya kundi la M23 na jeshi la FARDC mashariki mwa Congo. Katika
taarifa iliyotolewa Jumapili jioni na wizara ya mambo ya nje ya Marekani
ililaani hatua ya waasi wa M23 ya kusababisha majeruhi ya raia na
kushambulia tume ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa MONUSCO na
kupelekea raia wengi kutoroka manyumbani mwao.
vikali katika siku ya tano ya mapigano mashariki mwa mji wa Goma.
|
Twiga wa Tanzania |
No comments:
Post a Comment