Tuesday, 10 September 2013

ALEX MASSAWE NI VIGUMU KUPONA








Msemaji wa jeshi la polisi nchini, SSP Advera Senso.
Haruni Sanchawa na Makongo Oging'
KUNA taarifa zilizonaswa na gazeti hili wiki iliyopita zinazosema kuwa mfanyabiashara maarufu nchini, Alex Siriamka Massawe  atarejeshwa nchini wakati wowote kuanzia sasa, hivyo ni vigumu kupona au kukwepa mkono wa sheria.


 
Alex Massawe.....
 Habari kutoka makao makuu ya jeshi la polisi  zinasema, Massawe hawezi kukwepa mkondo wa sheria kwa kuwa tayari Polisi wa Kimataifa (Interpol) imekamilisha taratibu za kumleta nchini.
“Mipango yote imekwenda sawa kilichobaki ni kujua siku ya kuja hapa Bongo wiki ijayo (wiki hii) na akifikishwa nchini ataunganishwa pamoja na Papa Msofe kutokana na tukio la mauaji ya Onesphory Kituli aliyekuwa mfanyabiashara wa madini,” kilisema chanzo chetu.


Papa Msofe.
Habari zinasema polisi wanaopambana na madawa ya kulevya nao wanamtafuta Massawe kutokana na tuhuma ambazo hawakuzitaja kuhusiana na idara yao, hali inayoashiria kuwa huenda anahusishwa na biashara hiyo haramu.
Msemaji wa jeshi la polisi nchini, SSP Advera Senso aliwathibitishia waandishi wetu kuwa Massawe atarejeshwa nchini wiki hii.
“Mchakato wa mfanyabiashara Alex Massawe kurejeshwa nchini umekamilika akitokea katika nchi za Falme za Kiarabu hivyo atafikishwa hapa  wakati wowote,” alisema Senso.



Licha ya kuhusishwa na kifo cha Kituli aliyeuawa kwa kupigwa risasi Oktoba 11, 2011 Magomeni Mapipa, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar na Papa Msofe pamoja na Makongoro Nyerere kuswekwa rumande kuhusiana na tukio hilo, Massawe ana kesi nyingine mahakamani ya kughushi nyaraka.Chanzo:www.globalpublishers.info

Twaga

No comments:

Post a Comment