Wiki iliyopita ulifanyika mkutano Mjini Mombasa na kuhudhuriwa na marais, Uhuru Kenyatta wa Kenya, Yoweri Museveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda, Pierre Nkurunzinza wa Burundi na Salva Kiir wa Sudan Kusini, lakini Rais Kikwete hakuhusishwa.
Rais wa Rwanda |
Rais wa Tanzania |
na waasi wa FDLR ili wamalize migogoro yao, uhusiano baina ya Tanzania na Rwanda umekuwa shakani.
Mwaka 1994, wanajeshi wa Kihutu na wanamgambo waliua watu 800,000 nchini Rwanda wengi wao wakiwa Watutsi.
Kwa sasa, Rwanda inatawaliwa na Serikali ya
Watutsi chini ya Rais Paul Kagame, huku makundi ya kijeshi ya Kihutu
yakifuatilia kwa mbali. Moja ya makundi hayo ni FDLR.
Uhusiano kati ya Tanzania na Rwanda kwa sasa
unaonekana kulegalega kutokana na kitendo chake kupeleka majeshi yake
kuungana na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa (UN) vilivyoko
Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika Jimbo la
Goma.
Chanzo cha Uhasama
Uhasama huo unatokana na Kundi la M23 linaloundwa
na wapiganaji wa Kitutsi likiaminika kusaidiwa na Rwanda na linapambana
na majeshi ya Serikali ya DR Congo. Hata hivyo, Rwanda inapinga
kuisaidia M23.
Kumekuwa na malumbano kupitia vyombo vya habari vya nchi hizo mbili huku kila upande ukirusha vijembe vya kumponda mwenzake.
Mbali na vijembe, hivi karibuni Rwanda imejitoa na
kuanza kuacha kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuingizia mizigo yake,
badala yake sasa imejielekeza Mombasa nchini Kenya.
Hali hiyo inaonyesha kuiathiri Tanzania hata
katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambapo katika mikutano ya hivi
karibuni ya wakuu wa nchi hizo, Rais Kikwete hakushiriki.
Mkutano huo uliofanyika wiki iliyopita mjini
Mombasa na kuhudhuriwa na marais, Uhuru Kenyatta wa Kenya, Yoweri
Museveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda, Pierre Nkurunzinza wa Burundi
na Salva Kiir wa Sudan Kusini walialikwa na kutuma wajumbe wao, lakini
bila kumhusisha Rais Kikwete ni moja ya dalili ya Tanzania kutengwa au
kuenguliwa.
Baada ya mkutano huo, marais hao wamezindua eneo
jipya la bandari ambalo litasaidia kuimarisha huduma ya kupakia na
kupakua mizigo.
Tanzania...kwanza |
No comments:
Post a Comment