Sunday 8 September 2013

KUKOSA KIFUNGUA KINYWA KUNAWEZA KUSABABISHA UGONJWA WA MOYO











 


Kwa afya yako
Kwa afya yako
Matokeo ya utafiti wa kisayansi uliofanywa na Harvard University na kuhusisha watu zaidi ya 27,000 kuhusu umuhimu wa kifungua kinywa kwa afya ya binadamuyameonyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kupata matatizo ya moyo ikiwa kama haupati kifungua kinywa asubuhi.

Wataalam hao wamesema kwamba kwenye uchunguzi wao wamegundua kwamba mtu asiyekula kitu chochote asubuhi na kusubiri kula mchana anaufanya mwili wake utumie nguvu nyingi kuliko kawaida kwa sababu ya kukosa chakula kwa masaa mengi jambo ambalo linaweza kusababisha mshtuko wa moyo kutokana na mwili kufanya kazi ukiwa hauna nguvu ya kutosha.

Aidha, kwa kawaida ya mwili na tabia ya binadamu pale unaposikia njaa unaitaji chakula, kwa hiyo unapokosa kula asubuhi na njaa ikaja kabla ya muda wa chakula cha mchana kuna uwezekano mkubwa wa kula vitu vyenye sukari kama chocolate, biscut au vinywaji baridi ukisubilia chakula cha mchana. Vitu hivi vya sukari navyo vina mchango mkubwa kwenye magonjwa ya kisukari na kunenepa ovyo ambapo vitu vyote hivi pia vina mchango mkubwa kwenye magonjwa ya moyo.

Utafiti huo ulihusisha watu ambao hivi sasa wana umri kati ya miaka 45-82 ambapo walifanyiwa utafiti kwa muda wa miaka 16. Watu 1,500 waliathirika na mshtuko wa moyo kwasababu ya kukosa kifungua kinywa. Wataalamu hawa wamemaliza kwa kusema watu wanaokosa kifungua kinywa wapo kwenye hatari ya 27% ya kupata magonjwa ya moyo.

Ngiri poli

No comments:

Post a Comment