Sunday, 15 September 2013

POLISI ...... WAHAMIAJI

POLISI ...... WAHAMIAJI HARAMU KUSAKWA 
KWENYE SALUNI NA NYUMBA ZA IBADA

nyumba za ibada
POLISI : WAHAMIAJI HARAMU KUSAKWA KWENYE SALUNI NA NYUMBA ZA IBADA

Katika kuhakikisha kuwa wahamiaji haramu wote wameondoka nchini au wamefuata taratibu husika zitakazowaruhusu kuishi nchini, Idara Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, imesema hakuna eneo watakaloacha ikiwemo kwenye nyumba za ibada. Hii inafuatia taarifa kuwa kuna baadhi ya makanisa na misikiti inatumika kuwahifadhi wahamiaji haramu kinyume cha sheria. 

Taarifa zilizothibitishwa na Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Hokororo, ni kwamba idara yake tayari imemkamata Mchungaji wa Kanisa la Kimataifa la Life Changer Chapel, lililopo Sinza ‘E’, Grace Dangana Omotok, ambaye ni raia wa Nigeria, kwa kosa la kukiuka masharti ya kibali chake ambacho hakimruhusu kumuingiza raia yeyote nchini lakini yeye amewaingiza raia wengine sita ambao wanaishi nchini kinyume cha sheria.

“Hatufikiri kukutana na kiongozi yeyote wa dini, tutaendeleza msako hadi Jiji la Dar es Salaam liwe na wahamiaji halali tu. Uamuzi wetu unatokana na kuwa baadhhi ya viongozi wa dini si waaminifu. Pia tuntazipitia saluni za kike na kiume ambazo nyingi zinadaiwa kuajiri wahamiaji haramu,” alisema Grace Hokororo

“Tunaomba sana wananchi wenye mapenzi na nchi yao watusaidie kushughulikia hili suala la wahamiaji harama kwa maana limekuwa na madhara mengi sana kwa Taifa letu. Huu msako ni endelevu, hata wakijificha wapi tutawakamata tu,” alisisitiza ofisa huyo.
saluni

No comments:

Post a Comment