Wanasayansi nchini Marekani wamegundua chanjo ambayo wanaamini itaweza
kuangamiza Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa binadamu. Katika majaribio ya
chanjo hiyo, wanasayansi hao wameelezea kuwa imeonyesha mafanikio kwa
kuangamiza kabisa virusi wanaofanana na VVU kwa nyani.
Shirika
la Utangazaji la Uingereza (BBC) limetaarifu kuwa baada ya kubaini hilo
sasa wamekusudia kufanya majaribio ya chanjo hiyo kwa binadamu.Taarifa
ya ugunduzi huu ilichapishwa kwenye jarida la kisayansi linaloitwa;
Nature, ambalo lilimnukuu
Mwanasayansi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba cha Oregon, nchini
Marekani akisema walijiridhisha kuwa chanjo hiyo iliangamiza virusi
vyote kwenye mwili wa nyani.
Virusi hao jamii yake inafanana
sana na VVU wanajulikana kama Simian Immunodeficiency Virus (SIV) ikiwa
na maana ni virusi vinavyosababisha upungufu wa kinga ya kujikinga na
maradhi kwa nyani.
Taarifa za kisayansi zinaonyesha kwamba SIV
ni virusi ambao wamekuwa wakienea kwa njia ya kujamiiana miongoni mwa
vizazi vya nyani na vilibadilika baada ya kuambukizwa kwa binadamu
vikawa vimezaa VVU.
Wanasayansi hao wanasema kati ya nyani 16
waliopewa chanjo hiyo, waliyoipa jina la Cytomegalovirus (CMV),tisa
walipona kabisa maradhi ya SIV.
Mtaalamu wa Taasisi ya Chanjo
na Jeni katika Chuo Kikuu cha Oregoni, ambaye alihusika kwenye utafiti
huo, Profesa Louis Picker, aliielezea chanjo hiyo kuwa ni ya kutia moyo
ukilinganisha na nyingine ambazo zimewahi kufanyika.
“Katika
chanjo nyingi ambazo ziliwahi kuonyesha mafanikio ya kuangamiza virusi
ni kwamba kuna baadhi ya seli virusi walibakia,” alisema Profesa Picker,
akifafanua: “Lakini kwa chanjo hii tulichunguza sehemu nyingi nyeti
katika mwili wa nyani tukagundua kwamba hakuna kirusi aliyebakia.”
Alisema chanjo yao wameiamini kutokana na uwezo wake wa kupenya maeneo
mbalimbali ya mwili kiasi kwamba siyo rahisi kirusi kubakia.
Wanasayansi hao walisema kwa kawaida nyani ambaye ameambukizwa SIV hufa ndani ya kipindi cha miaka miwili.
Wanasayansi nchini Marekani wamegundua chanjo ambayo wanaamini itaweza
kuangamiza Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa binadamu. Katika majaribio ya
chanjo hiyo, wanasayansi hao wameelezea kuwa imeonyesha mafanikio kwa
kuangamiza kabisa virusi wanaofanana na VVU kwa nyani.
Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limetaarifu kuwa baada ya kubaini hilo sasa wamekusudia kufanya majaribio ya chanjo hiyo kwa binadamu.Taarifa ya ugunduzi huu ilichapishwa kwenye jarida la kisayansi linaloitwa; Nature, ambalo lilimnukuu
Mwanasayansi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba cha Oregon, nchini Marekani akisema walijiridhisha kuwa chanjo hiyo iliangamiza virusi vyote kwenye mwili wa nyani.
Virusi hao jamii yake inafanana sana na VVU wanajulikana kama Simian Immunodeficiency Virus (SIV) ikiwa na maana ni virusi vinavyosababisha upungufu wa kinga ya kujikinga na maradhi kwa nyani.
Taarifa za kisayansi zinaonyesha kwamba SIV ni virusi ambao wamekuwa wakienea kwa njia ya kujamiiana miongoni mwa vizazi vya nyani na vilibadilika baada ya kuambukizwa kwa binadamu vikawa vimezaa VVU.
Wanasayansi hao wanasema kati ya nyani 16 waliopewa chanjo hiyo, waliyoipa jina la Cytomegalovirus (CMV),tisa walipona kabisa maradhi ya SIV.
Mtaalamu wa Taasisi ya Chanjo na Jeni katika Chuo Kikuu cha Oregoni, ambaye alihusika kwenye utafiti huo, Profesa Louis Picker, aliielezea chanjo hiyo kuwa ni ya kutia moyo ukilinganisha na nyingine ambazo zimewahi kufanyika.
“Katika chanjo nyingi ambazo ziliwahi kuonyesha mafanikio ya kuangamiza virusi ni kwamba kuna baadhi ya seli virusi walibakia,” alisema Profesa Picker, akifafanua: “Lakini kwa chanjo hii tulichunguza sehemu nyingi nyeti katika mwili wa nyani tukagundua kwamba hakuna kirusi aliyebakia.”
Alisema chanjo yao wameiamini kutokana na uwezo wake wa kupenya maeneo mbalimbali ya mwili kiasi kwamba siyo rahisi kirusi kubakia.

No comments:
Post a Comment