Wednesday, 4 September 2013

Rwanda yajitetea kuhusu ushuru


HIFAGHI ZA WANYAMA



Dar es Salaam/Dodoma. Wakati ushuru wa magari makubwa ukiwa umeshushwa kwa wiki moja, Serikali ya Rwanda imejitetea ikisema haijafanya hujuma yoyote dhidi ya Tanzania, bali imepandisha tozo hiyo ili kuifanya ilingane na ile inayolipwa Tanzania.
Maroli ya... Tz
Maroli ya... Tz
Akizungumza na mwandishi wetu ofisini kwake jana, Balozi wa Rwanda nchini, Ben Rugangazi alisema kuongezwa kwa ushuru huo wa forodha
kisichukuliwe kama jaribio la kutaka kuvuruga uhusiano kati ya nchi hizi mbili.
Balozi Rugangazi alisema Rwanda imeamua kupandisha kiwango chake kutoka Dola za Marekani 152 (Sh240,000) kuwa Dola 500 (Sh790,000) ambazo pia hutozwa na Serikali ya Tanzania kwa muda mrefu.
“Kumekuwa na majadiliano ya muda mrefu ili kuleta ulinganifu wa ushuru wa forodha kwani kwa muda mrefu wafanyabiashara Rwanda wamekuwa wakilalamika kutokana na kushindwa kushindana vizuri kwenye soko la biashara kutokana na tofauti kubwa ya ushuru wa forodha.
“Hili suala tulishawahi kuliwasilisha katika Jumuiya ya Afrika Mashariki tukawaomba wasaidie kurekebisha kasoro hiyo, lakini hawakufanya hivyo. Sasa tumeamua kuchukua hatua hii ili kwenda sambamba na wenzetu Tanzania.
“Pande zote Tanzania na Rwanda zilikubaliana kuwa ushuru mpya ungeanza kutumika Septemba mwaka huu na ndivyo ilivyokuwa,” alisema Balozi Rugangazi.
Siku saba
Kutokana na msongamano wa malori kwenye mpaka wa nchi hizo mbili, Serikali ya Rwanda imeshusha ushuru kwa wiki moja.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba alisema ushuru unaotumika ni ule wa zamani badala ya mpya.
Tizeba alisema alishauriana na Waziri wa Miundombinu wa Rwanda, Profesa Silas Rwakabamba na kukubaliana ushuru wa zamani utumike wakati Serikali hizo zikiendelea na mashauriano. Alisema Mawaziri wa Fedha wa Tanzania na Rwanda walitazamiwa kukutana ili kuzungumzia suala hilo.
Dk Tizeba alisema juzi wafanyabiashara wa Tanzania walipata usumbufu mkubwa baada ya kulazimika kulipa Dola 500 kuingiza mizigo yao Rwanda badala ya Dola 152.
Hata hivyo, alikanusha madai kuwa Rwanda imepandisha ada hizo kutokana na mgogoro wa kisiasa baina ya nchi hizo.
MWEWE
1 | 2 Next Page»

No comments:

Post a Comment