SADC : KAGAME UKIISHAMBULIA TANZANIA,
TUTAKUPIGA
Nimekasilika |
Oparesheno kimbunga |
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imetoa onyo kali kwa Rais
wa Rwanda, Paul Kagame, kwa kumtaka aachane mara moja na na fikra
zozote mbaya alizonazo ikiwamo mipango yake ya kuihujuma Serikali ya
Tanzania na watu wake.
Onyo hili limefuatia nchi wanachama wa
SADC kufuatilia kwa makini mzozo wa kidiplomasia ambao Kagame aeuiubua
na amekuwa anaukuza hadharani na kichinichini dhidi ya Rais Jakaya
Kikwete na Tanzania kwa ujumla.
Habari hizi zimetolewa na viongozi wa juu wa SADC na maofisa wa
Serikali, waliokuwa katika ujumbe wa Rais Jakaya Kikwete alipokwenda
kuhudhuria Mkutano wa viongozi wa Maziwa Makuu huko Uganda hivi
karibuni. Aidha, imethibitishwa kuwa tayari Jumuiya hiyo imekwisha
mpatia ujumbe huo mmoja wa mawaziri aliyekuwa ameandamana na Kagame muda
mfupi baada ya kikao chake na Kikwete.
Kiongozi mmoja wa juu
wa Msumbiji ambaye alikuwa pia Uganda, alikaririwa akimueleza Waziri
aliyeandamana na Kagame kuwa “Nchi za SADC zinafahamu kuwa Rais Kagame
hajafurahishwa na uamuzi wa Tanzania wa kupeleka vikosi vyake Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo DRC. Hata hivyo Kagame anapaswa kuelewa kuwa
ilichofanya Tanzania ulikuwa ni msimamo wa pamoja wa nchi za SADC."
Aidha Kiongozi huyo aliendelea kusema "hivyo basi vitisho au uvamizi wa
kijeshi dhidi ya Tanzania utachukuliwa ni uvamizi dhidi ya SADC, na
tutakuwa tayari kuingia vitani kupigana upande wa Tanzania.”
Tamaduni za Africa |
No comments:
Post a Comment