Alex Massawe, mfanyabiashara maarufu nchini, anayetuhumiwa kushiriki
mauaji ya mfanyabiashara Onesphory Kituly ambaye aliuawa katika
mazingira ya kutatanisha Novemba 6, 2011 akiwa nyumbani kwake Magomeni -
Dar es Salaam, amefikishwa mahakamani Dubai, Falme za Kiarabu (UAE)
baada ya Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Polisi la Kimataifa
(Interpol) kuiomba Serikali ya nchi hiyo kumkamata.
Hivi
karibuni, Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu Dar es Salaam ilitoa hati ya
kukamatwa na kurejeshwa nchini kwa Massawe ili kukabiliana na kesi mbili
ikiwamo ya madai ya kughushi nyaraka mbalimbali.
Kufuatia hatua hii, Alex Massawe anatarajiwa kuletwa nchini wakati
wowote kuanzia sasa. Kukamatwa kwake kumekuja baada ya Polisi wa
Tanzania kumtafuta kwa muda mrefu bila mafanikio hadi mapema mwezi Julai
2013 ambapo maofisa wa usalama wa UAE walimkamata kwenye Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Dubai akitokea Afrika Kusini baada ya alama zake
za vidole kuonyesha kuwa alikuwamo kwenye orodha ya watu waliokuwa
wanasakwa na Interpol.
Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI),
Kamishna wa Polisi, Robert Manumba amethibitisha kuwa “Massawe
alifikishwa mahakamani Dubai kwa makosa ya kukutwa na hati tatu bandia
za kusafiria zilizokuwa na majina tofauti wakati alama zake za vidole
zilionyesha anaitwa Alex Massawe, lakini vilevile aligundulika kuwa ni
kati ya watu wanaotafutwa na Polisi wa Interpol kwa tuhuma za mauaji,”
alisema Manumba.
Alex Massawe, mfanyabiashara maarufu nchini, anayetuhumiwa kushiriki mauaji ya mfanyabiashara Onesphory Kituly ambaye aliuawa katika mazingira ya kutatanisha Novemba 6, 2011 akiwa nyumbani kwake Magomeni - Dar es Salaam, amefikishwa mahakamani Dubai, Falme za Kiarabu (UAE) baada ya Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol) kuiomba Serikali ya nchi hiyo kumkamata.
Hivi karibuni, Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu Dar es Salaam ilitoa hati ya kukamatwa na kurejeshwa nchini kwa Massawe ili kukabiliana na kesi mbili ikiwamo ya madai ya kughushi nyaraka mbalimbali.
Kufuatia hatua hii, Alex Massawe anatarajiwa kuletwa nchini wakati wowote kuanzia sasa. Kukamatwa kwake kumekuja baada ya Polisi wa Tanzania kumtafuta kwa muda mrefu bila mafanikio hadi mapema mwezi Julai 2013 ambapo maofisa wa usalama wa UAE walimkamata kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai akitokea Afrika Kusini baada ya alama zake za vidole kuonyesha kuwa alikuwamo kwenye orodha ya watu waliokuwa wanasakwa na Interpol.
Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna wa Polisi, Robert Manumba amethibitisha kuwa “Massawe alifikishwa mahakamani Dubai kwa makosa ya kukutwa na hati tatu bandia za kusafiria zilizokuwa na majina tofauti wakati alama zake za vidole zilionyesha anaitwa Alex Massawe, lakini vilevile aligundulika kuwa ni kati ya watu wanaotafutwa na Polisi wa Interpol kwa tuhuma za mauaji,” alisema Manumba.
No comments:
Post a Comment