Saturday, 14 September 2013

WKIENDI YENYE FURAHA.....(CHEKA)



 
Nyani


matibabu
Ha haaa konda kajinyea kitandani!!!!!!!!!!!
Konda alikuwa kakasirika sana, abiria alikuwa kagoma kulipa nauli akisisitiza eti yeye ni denti, wakati kila mtu alimuona ni mtu mzima, konda akamkunja jamaa, wakapigana sana, abiria alipoona anapigwa akaanza kukimbia, konda akamfukuza abiria akaaingia kwenye shimo, konda alipofika pale akakuta yeye hawezi kuingia kwenye shimo, kwa kisirani akaamua amkojolee humohumo kwenye shimo, wananchi waliokuwa karibu wakamhamasisha konda, 'Mnyee huyo, konda mnyee', konda akavua suruali na kulenga lile shimo na kuachia kitu. Hapo ndipo sauti ya hasira ya mkewe ikamuita, ikiambatana na makofi, konda akazinduka toka usingizini, akakuta kishaharibu mambo  yote kitandani.

Vichaa wawili
Vichaa wawili walipanga mkakati wa kutoroka kutoka hospitali ya vichaa Mirembe.
Mpango wao ulikuwa kwamba asubuhi ya siku inayofuata waende getini wamvamie mlinzi wampige wafungue geti watoroke.

Kesho yake asubuhi wakaamka mapema kama walivyopanga wakaelekea getini lakini kwa bahati mlinzi hakuwepo na geti lilikuwa liko wazi. Vichaa hao wakasikitika sana na kuambizana.
Haaaa, mpango wetu umeharibika mlinzi hayupo twende tutajaribu siku nyingine.

       Majina ya wauza Unga maarufu wa JF
Kwa kua viongoz wa nchi wanaogopa kuwataja wahusika wanaojihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya...Nachukua fursa hii kwa ujasili mkubwa na tena nikiwa na uhakika wa asilimia mia kuwataja wahusika ambao wamo katika folamu hii ya jamii.


1. Mamdenyi

Huyu anamiliki majumba ya anasa. Ana rosheni pale kariakoo kama 4 ivi na anadalala zinazopiga ruti Mwenge posta zaidi ya 30.

2.Lara1

Huyu kijana mdogo kabisa lakini machachari. Mara nyingi amekua akiongozana na Riz1. Anapenda kutembelea gari aina ya vogue nyekundu na pia ndiye mwenye jengo jipya kama unaelekea posta limeandikwa VIVA..maeneo ya redcross. Mara nyingi amekua akifanya matanusi zanzibar na kusafiri mara kwa mara nje ya nchi. Ana vitega uchumi vingi sana hapa mjini na ana share 80% ya vodacom.

3. Heaven on earth


Huyu richa ya umaarufu alionao.anamiliki ukqasi mrefu sana. Mara ya mwisho alijitangaza anapesa zinazozidi bilion 90 kwenye account yake. Anapenda sana kuhudhuria kwenye bendi za taarabu hasa ya mashauzi claasic ambapo huwatunza kwa hela nyingi sana. Ndiye mmiliki wa bajaji zote za mwenye na ile stand ya makumbusho.

4. Watu8

Jamaa anapenda kubadilisha magari na wanawake kila saa. Ni mtoto wa kigogo. Mara ya mwisho alikamatwa South Africa na kuachiwa kimya kimya but ilisemekana alihonga tirion 2 za kibongo. Yeye ndio mtanzania mwenye gari la gharama kuliko wote hapa tz.

Uongo mwingine hataa haufai
UONGO MWINGINNE HATA HUFAI!
jamaa:unasoma?
demu:sisomi,vipi wewe unasoma?
jamaa:ndio nipo kidato cha nne roleto.
demu:jamani hiyo si ni shule ya wasichana?
jamaa:aaah nimechanganya nipo ngaza
demu:mweeembona nayo ya wasichana
jamaa:ha! ha! ha! nilikuwa nakutania tu nachukua masters VETA.
demu:mh ina maana VETA imeanza kutoa masters?
jamaa:ishia zako demu mwenyewe hulipi wala nini unaniuliza maswali kama tuko uhamiaji?
KWA TAARIFA NACHUKUA DEGREE YA UDAKTARI CBE

Nyani

No comments:

Post a Comment