Saturday, 21 December 2013

Hakuna mwaka mbaya, ubaya unao mwenyewe



HAKUNA MWAKA MBAYA
Jamani naona mwaka unaisha huku kila mtu akisema lake. Aliyelia
MWAKA MBAYA UNAO WEWE MWENYEWE
kalia na aliyecheka kacheka, lakini wale wa kulalamika pia tunao. Utasikia; Oooh, mwaka haukuwa mzuri kwangu.
Mbona wenzio walifanikiwa?
Mwenzenu nina imani moja kuhusu maisha haya ya kubahatisha, yanayotegemea mwaka mbaya na mzuri. Naamini kabisa ya kwamba, hizi bahati huendana na jitihada. Yaani jitahidi kufikia kwenye mafanikio siyo kukaa kibarazani kwako unasubiri mafanikio yakufuate.
Saa ngapi, nani kakwambia kwamba yanakujaga miguuni na kujivalisha kama viatu?
Jipange; mjue kuna wakati mimi hukaa na kujiuliza; hivi kwa mfano tusingetawaliwa na wazungu au waarabu, hizi tarehe au miaka zisingekuwepo. We ungeujuaje mwaka mbaya na mzuri?
Ukifikiria kwa makini, utagundua kwamba hizi ni kauli za kujibaraguza zilizozoeleka kwenye jamii ya wasiojishughulisha a.k.a watu wa kutafuta sababu za kukubali kushindwa maisha.
Vijana wenzangu, naomba niwakumbushe kwamba; kukata tamaa ndiyo chimbuko la kushindwa kwetu kufikia katika mafanikio. Tusikariri maisha, Tanzania bado kubwa na kushindwa leo siyo kushindwa kesho, bali kushindwa leo ni somo zuri kwa ajili ya mchezo wa kesho.
Mnanielewa?
Msichukulie matatizo yanayotukumba kila siku, kama sababu ya kuacha mapigano, bali tuyachukulie kama ni mafunzo kwa ajili ya vita ya kesho.
Ulipokwama jana, leo usipite, pita kwingine au safari hii pita ukiwa na zana za kujikwamua.
Mnanielewa?
Kama mnaelewa sawa, mwaka umeisha, kulalamika siyo suluhisho, tuangalie mwakani kutakuwa na nini, ili tuendeleze mapigano. Ulipokwama mwaka huu pageuze kuwa darasa, pakusaidie katika upambanaji wako wa mwakani.
1 | 2

MBUNI..

No comments:

Post a Comment