Thursday 2 January 2014

BWIMBWI LAWATESA WATANZANIA....HUKO MAJUU.

 

 

 

HATIMAYE SUPER STAR RAY C AFUNGUKA

 NA KUMCHANA LIVE JACKIE

 CLIFF SOMA ALICHOSEMA!!




ray2

ray-c
Hivi karibuni aliyekuwa msanii wa Bongo Fleva na Radio presenter, mwana dada Rehema Chalamila maarufu kwa jina la Ray C, aliingia katika mjadala mkubwa na mashabiki wake katika mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya kupost picha ya mrembo Jackie Cliff aliyekamatwa nchini China kwa kosa la kusafirisha madawa ya kulevya jijini Macau nchini humo, na kutoa yake ya moyoni kutokana na tukio hilo.

Post ya mwana dada Ray C ilizua mjadala mkubwa katika mtandao wa huo wa Instagram kiasi cha kwamba, fans wake walimpa support kutokana na kauli yake ya kutaka Jackie auwawe tu, huku fans wake wengine wakimsihi asimuombe mabaya mrembo huyo aliyekamatwa. Ray C alitoa kauli hiyo kutokana alishawahi kuwa muathirika wa madawa hayo kipindi cha nyuma na kusema kuwa watu wanaojihusisha na biashara hiyo haramu hawana huruma kwa hiyo na yeye hawaonei huruma hata kidogo kwa sababu walimfanya ateseke yeye na familia yake kipindi alipokuwa muathirika wa madawa ya kulevya.
 
 

No comments:

Post a Comment