Abiria wa Tanzania akamatwa Hong Kong
Abiria wa Tanzania akamatwa Hong Kong na
heroin ikiwa ndani ya mashine
Kwa mara nyingine, maafisa wa Hong Kong katika kiwanja cha ndege
wamefanikiwa kukamata dawa za kulevya zilizokuwa zinasafirishwa kutokea
Tanzania safari hii zikiwa zimefichwa katikati ya chuma cha mashine.
Dawa hizo aina ya heroin zilikamatwa katika nyakati mbili tofauti kwa
jumla zikiwa na kilo 1.5 na thamani ya dola milioni 1.3 za Marekani.
Maafisa hao wanasema kwa kuwa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu nyendo za
wauza dawa na mbinu za kuficha dawa hizo, walilazimika kukikata chuma
cha mashine hiyo ili kuziona.
Adhabu ya kupatikana na dawa za kulevya huko Hong Kong ni faini ya dola milioni 5 za Kimarekani.
Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Serikali ya nchi hiyo na picha zinazoambatana na taarifa hiyo vimepachikwa hapo chini.
No comments:
Post a Comment