NISEME UA NISISEME.?
 Ndugu Mwanasheria kwama ulivyo dai wa BUKOBAWADAU Blog..Ninayo heshima kuchangia katika hoja yako uliyo
iandika kuhusiana na Tamko la kuwaamuru Raia wa Nje ambao hawafuatu sheria
ndani ya Tanzania kurudi makwao au uwepo wao ni kinyuma cha sheria ….
Ndugu Mwanasheria kwama ulivyo dai wa BUKOBAWADAU Blog..Ninayo heshima kuchangia katika hoja yako uliyo
iandika kuhusiana na Tamko la kuwaamuru Raia wa Nje ambao hawafuatu sheria
ndani ya Tanzania kurudi makwao au uwepo wao ni kinyuma cha sheria ….
Sasa tangu kauri hiyo
ya kuwaamuru Wahamiaji haramu/Wahamiaji wasio rasmi  kutamkwa zaidi ya watu  wapatao 
8,000 wamekwisha rudi katika nchi zao walizo tokea huu ni Utii wa ndugu zetu
na ueleo wa Sheria kwani kuingia kwao nchini kulikuwa ni batili si harali…
Walivamia aidha
kwakufahamu au kwakuto fahamu (Sheria) sisi tungependa kusema yakuwa hili ni
jambo zuri na nivyema watakapo hutaji kurudi nchini warudi kwa kufuata sheria ….za
uingiaji nchini (Idara ya Uhamiaji) , Idara ya Ardhi, Idara ya Mifugo….zifuate
sheria zanchi katika kudhibiti wa wageni aidha katika “Nyanja zao HAKIKA
TUTAKUWA TUME TENDEA HAKI MAAGIZO YA SEREKALI” Katika kupambana na wahamiaji
wasio Rasmi…..hususani majambazi kutoka nje ya nchi.
Sasa lengo la kuyasema haya ni kwamba huenda baadhi ya
wananchi na hata wageni wanao vuka mipaka ya nchi yetu ya Tanzania kutokuwa na
ufahamu wa Tanzania kunasherika wanacho kifahamu tuu kuwa Jeshi la Police
kukamata na kuweza kukushughulikia kwa mujibu wa sheria na kusahau yakuwa Idara
nyingine nazo zina majukumu yao kitaifa ya kuweka ulinzi wa taifa leti 
Tazama sasa Wageni walijibwetekeza kiasi cha kuhodhi Ardhi…Kuingiza
Mifugo, Ukataji miti mapolini kiholela, Uuaji wanyama hovyo, Uvamizi wa
madaraka kihorela…..wenyeviti wa vitongoji, Wenyeviti wa vijiji, Udiwani  Ubunge nk. Kwakweli hili ni kosa kwani hata
katiba ya nchi yetu sidhani kama itakubali hili …Ardhi, Uongozi , uhodhiwe na “WAGENI
WASIO RASMI”….
SHERIA ZA UHAMIAJI ZINASEMAJE:
| SHERIA ZA UHAMIAJI | 
Katika Idara ya Uhamiaji kuna sheria zinazi ongoza utendaji
kazi zake  na ndio maana kuna wataalamu
wa masiala ya Kiuhamiaji nk.
·        
Sheria za
Uhamiaji,
·        
Sheria za
Uraia, 
·        
Sheria za
Passport.
·        
Sheria Nyingine
ni za mashitaka,
·        
 Zamakosa ya jinai,
·        
Na za ushahidi.
Leo nitazingumzia sheria za Uhamiaji  kwa kifupi na zoezi hili linalo endelea zina
mahisiano gani:
Kwakweli mgeni yeyote anapo adhimia kuingia nchini ni lazima
afuate sheria  afike na kuripoti katika
Ofisi za uhamiaji na kutoa adhima yake ya kuingia nchini au kutoka nchini na
kujaza fomu ya uingiaji au utokaji nchini nikiwa na maana TIF.10 & 11
(itakayo hoji majina, Passpot, Utaifa, Dhumuni, nk. La safari yako ya kuingia
nchini au kutoka nchini…..”usipo fanya hivyo na ukajikuta aidha umeingia au
umetoka nchini uwepo wako utakuwa tayari umevunja sheria …..”
Hivyo basi  wageni wengi walio
kumbwa na zoezi hili ni wale ambao wakati wameingia nchini na kuendelea kishi
nchini  na walishindwa kuhalalisha uwepo
wao nchini aidha waliingia kwa njia za panya au baada ya kuingia hawakuendelea
tena kufuata taratidi za kuishi nchini kwa kuomba vibali vya kuwahalalishia
akaaji/uwepo wao nchi…….utaona  wageni
hawa baada ya kuingia nchini na kukaa katika tabia za kujificha kwa kujifunza
kuzungumza kuswahili ama lugha za ndani ya Tanzania pia wengi wao wamo nchini
zaidi ya miaka 40  na tayari wemekwisha
jukuu  na kutukuu napengine hata
kushikilia nyazifa mbalimbali nchini au serikalini hii ni hatari
Lakini hebu tuone hivi Sheria ya Uraia inasemaje kwakweli
Raia wa Tanzania ni Yule Mzaliwa wa Tanzania na Mmoja wa wazazawake ni Raia wa
Tanzania au wote, Raia wa Tanzania kwa kuridhi ..Pengine wewe ulizeliwa nje ya
nchi na mmoja wa zazi wako ni Raia wa Tanzania hivyo baada ya kufikisha miaka 18
unapaswa kuu kana ule uraia wan chi ya nje uliyo zaliwa….na kuna Uraia wa
Tajinisi yani wewe ulikiwa Raia wanchi furani na ukaamua kuja na kuishi
Tanzania Kwa kufuata sheria kwa kuwa na Passporti  iliyo hai ya nchi yako ulikuwa na vibali vya
ukaaji  vilivyo hai na tayari umekwisha
fikusha miaka kumi (10) ndani ya Tanzania na ukaomba maombi ya uraia kuanzia
ngazi ya chini ya serikali, ukaja wilayani,  mkoani, ukaenda hadi Taifani …na wazili wa
mambo yandani ya nchi na akakukubalia kwani yeye ndiye mwenye uwezo /kauli ya
mwisho katika utoaji wa uraia huu wa Tajinisi….
ANGALIZO:
Tunawaombeni sana mtoe ushirikiano katika hili zoezi la
kuwabaini wahamiaji haramu au wasio Rasmi….
Tungependa ndugu yetu
mwanasheria kama ulivyo jitambulisha  uzipate
sheria za Uhamiaji ili muwe na ueleo wa masuala ya kiuhamiaji  kwani nawewe ni mmoja wa wadau wanchi yetu….
AHSANTENI


No comments:
Post a Comment