SIMO NA NJERO |
AFYA YA NGOZI :
Hamira;
jamii ya fangasi wenye madhara mwilini
Katika mwendelezo wa makala yetu ya maradhi ya ngozi tunaendelea kuangalia maradhi ya ngozi yatokanayo na fangasi, leo tukiangalia hamira (yeast) yanavyoshambulia sehemu mbalimbali za mwili. Maradhi haya kitaalamu huitwa tinea versicolor.
Utango tango (mba)
Mba ni maradhi maarufu zaidi kati ya magonjwa mengi yanayosambazwa na fangasi wanaoitwa Malassezia furfur ambao kwa kawaida huishi kwenye ngozi ya watu wazima bila kusababisha matatizo yoyote ya kiafya.
Vimelea hivi husababisha ngozi kwenye sehemu ndogo
ya mwili kubadilika rangi ukilinganisha na rangi ya ngozi ya sehemu ya
mwili iliyoizunguka.
Mba hushambulia nani?
Kwa kawaida, maradhi haya hushambulia zaidi vijana walio katika umri wa balehe na watoto.
Mwonekano wake
Maradhi haya hutambulika kwa namna mbalimbali, lakini ya muhimu zaidi ni mwonekano wake. Hutambulika kitaalamu kama ‘versicolor.,
neno la Kigiriki linalomaanisha kubadilika kwa rangi ya ngozi na hii
humaanisha kuwa sehemu ya ngozi inayopata maambukizi ya maradhi haya
hubadilika rangi yake kutoka ile ya asili.
Mfano rahisi ni mabadiliko ya rangi ya ngozi
kutoka maji ya kunde na kuwa nyeusi zaidi au nyeupe zaidi ukilinganisha
na sehemu za ngozi zilizozunguka eneo lenye maambukizi ya fangasi hao.
Ni sehemu gani hushambuliwa?
Maeneo ya ngozi yanayoathiriwa zaidi katika mwili ni mabega, shingo, mgongo na kifua.
Mara nyingine maradhi haya hushambulia maeneo
ngozi inapojikunja kama vile maungo ya mikono, ngozi ya chini ya matiti,
maeneo ya siri hasa pale miguu inapoanzia.
Uso mara nyingi hauathiriki, ingawa kwa watoto wanaweza kupata maambukizi ya kwenye kidevu, pua, mashavu na hata paji la uso.
Mara nyingi, fangasi hawa wanaposhambulia uso
hushambulia kwa wingi kiasi kwamba ukimtazama mgonjwa kwa haraka haraka
unaweza kudhani kuwa hiyo ndiyo rangi yake halisi ya ngozi na kuwa
maeneo ambayo hayajaathirika ndiyo yaliyoathirika.
Sababu za kutokea kwake
Sababu za maradhi haya bado zinafanyiwa uchunguzi,
lakini kama nilivyosema kwenye makala za nyuma kuhusu namna fangasi
wanavyosambaa, na kwamba, sababu hizi pia ni muhimu, nazo ni;
-Hali ya majimaji kwenye ngozi (inaweza kuwa hata jasho)
-Hali ya hewa ya joto (fangasi wanakua vizuri kwenye hali ya joto)
-Kinga ya mwili ikiwa chini
-Mabadiliko ya homoni
Inawezekana pia maradhi haya kupata watu ambao wamekosa sababu zilizotajwa hapo juu.
Usambaaji wake
Kwa vile vimelea vya fangasi vinavyosambaza
maradhi haya kwa hali ya kawaida huishi kwenye ngozi si lazima mtu
aambukizwe, bali kwa kawaida maradhi haya hutokea tu.
No comments:
Post a Comment