HIZI NI NOMA....HEBU CHEKA UPASUKE hahahahaaaah! |
Huu ni utani au kweli?
Mzee mmoja aliongozana na binti yake kwenda kwa mwanaume aliyempa mimba huku akitweta kwa hasira. Walipofika ilikua hivi: Mzee,wewe ndio ulimpa mimba bint yangu?
KIJANA: Mzee ni kweli mimi nimempa mimba binti yako, ila akizaa wakiume nitakupa daladala 3, sheli 1 na milioni 50 za mtaji. Akizaa wakike, nitakupa supermarket 1, mashamba 2 na milioni 40.
BINTI AKADAKIA: Je mimba ikitoka?
MZEE: Nyamaza mshenz ww, si atakupa nyingine...
chezea pesa?
Hivi itakuwaje shetani akiokoka?
Maranyingi shetani hulaumiwa kwa mambo mengi..watu baada ya usalitiana utamskia msaliti akidai "nisamehe ni shetani tu alinipitia", yakitokea mauaji yyte ya kinyama utaskia watu wanadai "shetani kawa na nguvu sn sikuhizi" watu wanafanya unyang'anyi, wizi, ufisadi, n.k. yote utaambiwa ni "shetani" Sasa akiokoka huyu "master wa uovu itakuwajee??" Mimi naona DUNIANI HAKUTAKUWA NA DILI KABISA HUYU JAMAA AKIOKOKA.Nani hapa anazingua wenzake?
Boss alimpigia simu secretary wake kwamba wanaenda trip wiki ijayo,secretary akampigia mme wake simu kwamba hatakwepo kwa wiki moja atakuwa yupo kwenye trip na boss.
mme wa secretary akampigia hawara wake simu kwamba aje nyumbani wawe pamoja mkewe kasafiri,hawara akampigia simu mwanafunzi wake anayemfundisha kwamba hatamfundisha mpaka baada ya wiki moja,mwanafunzi akampigia simu babu yake (boss),kwamba hamna shule kwahiyo atakuja nyumbani kwa wiki mmoja,boss akampigia simu secretary wake kwamba hamna trip tena,secretary akampigia mmewe kwamba trip imeahirishwa,mme akampigia simu hawara kwamba asije mmke kaahirisha safari,hawara akampigia mwanafunzi wake kwamba shule ipo kama kawaida,mwanafunzi akampigia babu(boss) kwamba siji tena shule kama kawaida ipo.Boss akampigia tena secretary kwamba tuna trip kama kawaida.
No comments:
Post a Comment