Mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC
Mahakama
ya kimataifa ya uhalifu, ICC imesitisha uamuzi wa kumruhusu naibu wa
rais wa Kenya, William Samoeio Ruto, kutohudhuria baadhi ya vikao vya
kusikilizwa kesi yake kuhusiana na machafuko ya baada ya uchaguzi wa
mwaka 2007, inayotarajiwa kuanza tarehe 10 mwezi ujao huko The Hague,
Uholanzi. Mwezi Juni mwaka huu mahakama hiyo ilisema Ruto angeweza
kukosa kufika mahakamani na kubakia Kenya kwa baadhi ya siku kuendelea
na kutekeleza majukumu yake. Lakini mwendesha mashtaka mkuu wa ICC,
Fatou Bensouda, alikata rufaa dhidi ya uamuzi huo akisisitiza Ruto
pamoja na mshtakiwa mwenzake, Joshua arap Sang, wawepo mahakamani wakati
wote wa kusikilizwa kesi yao. Jopo la mahakama lilibatilisha uamuzi huo
jana kusubiri matokeo ya rufaa ya Bensouda. Je unauonaje uamuzi huo?
No comments:
Post a Comment